August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wavamizi mwendo kasi kukiona

Spread the love

MOHAMMED Mpinga, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani amesema, Jeshi la Polisi halitatoa adhabu ya kulipa faini kwa madereva wa vyombo vya moto watakaopita barabara ya mabasi ya mwendokasi badala yake watafikishwa mahakamani, anaandika Hamisi Mguta.

Hayo ameyaeleza leo katika mkutano na waandishi wa habari alipozungumza kuhusu hatua zitakazochukuliwa na jeshi hilo kwa madereva wanaotumia njia ya mabasi hayo.

Kamanda Mpinga amesema, tangu mei 10 safari za mabasi ya mwendokasi zilipoanza, jumla ya ajari 14 zimetokea na kuhusisha mabasi ya mwendo kasi na magari ya watu binafsi.

“Kuaniza tarehe 1 mwezi wa 6 hadi tarehe 6 mwezi 6, jumla madereva 33 wamekamatwa katika njia ya BRT Kinondoni huku bodaboda zikiwa 29 na magari binafsi 4;

“Ilala, madereva 21 wamekamatwa katika barabara ya BRT mbapo bodaboda 19, wawili magari binafsi,” amesema.

Amesema, tayari madereva wawili wa bodaboda kati yao, Hassan Muhamed, Mkazi wa Tegeta na mwenzake Rashid Sheha, Mkazi wa Kimara wamehukumiwa kifungo cha miezi sita,” amesema Mpinga na kuongeza;

“Jeshi la Polisi linafanya oparesheni kali ya kuwakamata wanaopita katika barabara hizo na kuhakikisha wanakaa maabusu na kesho yake kupelekwa mahakamani, hakuna kulipa faini, wala dhamana kwasababu tumegundua tukiwapa dhamana wanakimbia.”

Aidha amesema, watakaokamatwa katika barabara hiyo watapigwa picha wakiwa wameshikiria kibao kinachoonesha jina lake, muda na kosa alilolifanya jambo ambalo litasaidia kuonesha uthibitisho kuwa, aliwahi kufanya kosa endapo atarudia tena.

error: Content is protected !!