August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wavamia kanisa watembeza ‘kichapo’, wapora

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza

Spread the love

KUNDI la watu wasiofahamika,  limevamia na kuvunja Kanisa la Mwanza City Center International Church Tanzania Reveland, lililopo Butimba mkoani Mwanza na kuanza kutembeza kichapo kwa walinzi na kuiba baadhi ya vifaa vya kanisa hilo, anaandika Moses Mseti.

Inaelezwa kwamba uongozi wa kanisa hilo ulikuwa na mgogoro na bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kanda ya ziwa, huku kikundi cha wahalifu hao kikidaiwa kufanya uhalifu huo Juni 27 mwaka huu saa 11 alfajiri.

Mama mzazi na Mchungaji wa kanisa hilo, Mama Moses Kulola ambaye ndiye mlezi wa Kanisa hilo, alisema alipigiwa simu na kuelezwa kuhusu kuvamiwa kanisa hilo huku akida  wavamizi hao walivunja ukuta na kuanza kuwapiga walinzi waliokuwa mlangoni.

Amesema kuwa baada ya kuanza kuwashambulia walinzi hao na kwamba walinzi hao walikimbia, na kuwapa nafasi ya kuingia ndani na kuiba viti, mabati na maiki zote, Spika na ngoma za kwaya zikibomolewa zote na wakatokomea kusikojulikana.

“Hii ni nyumba ya Mungu, najua heri ubomoe nyumba yangu mimi binafsi lakini nyumba ya Mungu ni jicho la Mungu, hapa watu wanakwenda kuabudu na kuombewa, matatizo yao yanaondolewa na Mungu, atakayeshughulika na hao waliobomoa ni Mungu sio sisi,” amesema Mama Moses Kulola.

Revocatus Deus, Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo,  amesema kuwa wakati wahalifu hao wanavunja ukuta wa kanisa kwa lengo la kuingia kupora mali, waliwajeruhi walinzi wa kanisa hilo akiwemo yeye mwenyewe sehemu mbalimbali ya miwili wake.

Michael Kulola, Mchangaji kiongozi wa Kanisa hilo, amewaomba waumini wawe na utulivu katika kipindi hiki suala hilo likiendelea kushughulikiwa na jeshi la Polisi ili kukibaini kikundi kilichofanya uhalifu huo kwenye nyumba ya mungu.

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, alithibitisha kuvunjwa kwa kanisa hilo huku akidai tayari jeshi la polisi limeanza uchunguzi  wa tukio hilo, lililofanywa na watu wasiofahamika.

Kulwa Steven, Msimamizi wa majengo wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kanda ya ziwa, alipotafutwa na Mtandao Huu, kupitia simu ya mkononi, kuzungumzia suala hilo ikiwa kama kweli walikuwa na mgogoro na kanisa hilo hakupatikana.

error: Content is protected !!