March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wauzaji kuku Singida wapaza sauti

Kuku wa kienyeji

Spread the love

WAFANYABIASHARA wa soko la kuku mkoani Singida wameiomba Serikali kuangalia na kuboresha upatikanaji wa masoko ya uhakika hapa nchini, anaandika Christina Haule.

Ombi hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa soko hilo, Shabani Mahiki wakati akizungumza na viongozi na waandishi kutoka klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (MoroPC) na Singida SingPress walipotembelea kwenye soko hilo kuona faida na manufaa wanayopata wafanyabaishara hao.

Mahiki alisema wafanyabiashara wanaosafirisha kuku kwenye matenga kwenda mkoa mbalimbali hasa jijini Dar es salaam wanunuzi wamekuwa siyo waaminifu.

“Utakuta mmetuma mzigo labda tenga zenye thamani ya shilingi milioni moja halafu mtu anapokea mzigo na baada ya wiki kadhaa anakutumia laki tano badala ta kukutumia zote,” amesema Mahiki.

Muuzaji wa kuku katika soko hilo, Jumanne Mkotya aliiomba Serikali kuondoa au kufuta ushuru kwa biashara ya kuku.
Mkotya amesema, usafirishaji wa kuku mikoani husababisha baadhi ya kuku kufa njiani.

error: Content is protected !!