Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waumini 26 wapigwa risasi kanisani Marekani
Kimataifa

Waumini 26 wapigwa risasi kanisani Marekani

Kikosi cha FBI kikifanya uchunguzi eneo la tukio
Spread the love

WATU 26 wameuawa kwa kupigwa risasi wakiwa kanisani na mtu mwenye silaha katika jimbo la Texas nchini Marekani walipokuwa katika ibada.

Shambulio hilo lilitekelezwa katika kanisa la First Baptist Church katika mji wa Sutherland Springs, mji mdogo katika wilaya ya Wilson, Texas.

Mshambuliaji, ambaye anadaiwa kuuawa baada ya kutekeleza mauaji hayo, aliingia kanisani na kuanza kuwafyatulia risasi waumini kabla ya yeye kuuawawa.

Gavana Greg Abbott amethibitisha idadi ya waliofariki na kusema ndicho kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutekelezwa kwa kutumia bunduki katika historia ya texas.

“Kutakuwa na majonzi na masikitiko mengi kwa wale walioathiriwa,” aliwaambia wanahabari.

Mkuu wa idara ya usalama wa Texas Freeman Martin amesema waathiriwa walikuwa na umri wa kati ya miaka 5 na 72.

Maafisa wamesema watu zaidi ya watu 20 pia walijeruhiwa na katika shambulio hilo na wamelazwa hospitalini.

Martin amesema mshukiwa ni mwanamume mzungu wa umri wa miaka 20 ambaye alikuwa amevalia mavazi meusi na fulana ya kujikinga dhidi ya risasi pamoja na kuwa na bunduki yenye uwezo mkubwa.

Alianza kufyatua risasi nje ya kanisa kabla ya kuingia ndani na kuendelea kufyatulia watu risasi.

Katika mapambanao hayo muumini mmoja alimnyang’anya bunduki na kuanza kumfyatulia ” risasi mshukiwa hatua iliyomfanya aanze kukimbia kwa kutumia gari lake.

Raia huyo alimwandama mshukiwa huyo ambaye aliendesha gari lake na kisha kuamua kuliangusha katika barabara wilaya ya Guadalupe.

Polisi walipofuatlia walimkuta mshukiwa akiwa amefariki ndani ya gari lake.

Hata hivyo, haijafahamika kama iwapo alifariki kutokana na majeraha ya risasi aliyojisababishia mwenyewe au kutokana na mejaraha kutoka kwa raia huyo, Martin ameongeza.

Mshukiwa huyo amefahamika kwa jina la Devin P Kelley (26), kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani.
Mhubiri wa kanisa hilo la First Baptist Frank Pomeroy, ameambia ABC News kwamba binti yake wa miaka 14 kwa jina Annabelle ni miongoni mwa waliouawa.

Sutherland Springs ni mtaa mdogo wenye wakazi wasiozidi elfu moja ambao hupatikana kilomita 50 hivi kusini mashariki mwa mji wa San Antonio mjini Texas.

Maofisa wa FBI kutoka San Antonio wametumwa kufanya uchunguzi ingawa mpaka sasa haijafahamika lengo la mshambuliaji huyo lilikuwa ni nini.

FBI pia wamesema mshambuliaji alikuwa peke yake, lakini bado wanachunguza uwezekano wa iwapo kuna mtu mwingine aliyehusika.

Rais Donald Trump, ambaye yupo ziarani Asia, ameshutumu kisa hicho na kusema ni “kitendo cha uovu” na kusema kwamba Wamarekani watajikwamua na kusalia na umoja.

“Kupitia kwa machozi na kupitia huzuni hii, tunasalia imara, imara zaidi,” ameongeza.

Mauaji hayo yametokea mwezi mmoja tu baada ya mshambuliaji mwingine kufyatulia risasi watu waliokuwa wakihudhuria tamasha la muziki Las Vegas na kuwaua watu 58 pamoja na kujeruhi mamia wengine.

Hili ni tukio baya zaidi la mauaji ya kutumia bunduki katika historia ya Marekani katika miaka ya hivi karibuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!