January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wauaji wa Dk. Slaa hawa hapa

Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, (CCM), Philip Mangula

Spread the love

ELISIFA Ngowi, naibu mkuu wa usalama wa taifa mkoa wa Dar es Salaam, ni miongoni mwa waliopanga mkakati wa kuangamiza maisha ya Dk. Willibrod Slaa. Anaripoti Deusdedit Kahangwa(endelea).

Ngowi ni mmoja wa watu 30 wanaotajwa kupanga njama za kumuua Dk. Willibrod Slaa kwa “…sumu au njia nyingine ambazo zisingegundulika.”

Kwa mujibu wa mawasiliano katika simu ya Khalid Kangezi, mmoja wa walinzi wakuu wa Dk. Slaa, aliyekiri kushiriki njama za kumuua mwanasiasa huyo shupavu, yanaonyesha orodha ndefu wakiwamo waliotajwa kuwa maofisa wa idara ya usalama wa taifa (TISS).

Ngowi ni mmoja wa watuhumiwa muhimu katika wizi wa fedha za umma katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). Alikwapua mabilioni ya shilingi kupitia kampuni yake ya Clayton Marketing Ltd na Excellent Services Ltd.

Kampuni ya Ngowi – Clayton Marketing Limited – ni miongoni mwa kampuni 22 yaliyochotewa na serikali kiasi Sh. 133 bilioni kutoka BoT.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Kangezi na baadaye kuwasilishwa kwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, Ngowi ni miongoni mwa waliopanga mkakati wa kumuua Dk. Slaa, ulitakiwa kutekelezwa kabla ya mwisho wa Aprili mwaka huu.

Mwingine anayetajwa kupanga njama za mauaji hayo, ni Philiph Mangula, makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara.

Kagenzi anasema, “Mpango wa kumdhuru Dk. Slaa niliuanza tangu tarehe 8 Julai 2014, tukiwa Kituo cha Demokrasia (TCD), Ilala Dar es Salaam. Mawasiliano haya nilianza kufanya kupitia kwa Burton Mn’gen’ge, ambaye ni msaidizi wa Mangula.”

Anasema, “Huyu bwana alinishawishi kuwa nampa taarifa za siri za chama, pamoja na Dk. Slaa binafsi. Watu hawa wamekuwa wakinipa fedha za muda wa maongezi ili kufanya mawasiliano nao na fedha nyingine kwa ajili ya matumizi mengine.”

Kangezi anataja namba mbili za simu yake ambazo zimekuwa zikifanya mawasiliano mfululizo na washirika wake kuwa ni 0764 367750 iliyosajiliwa kwa jina la Sudi Juma na 0763 848530 iliyosajiliwa kwa jina la Khalid Kangezi.

Namba nyingine ya Kangezi ni Na. 0652 215875 ambayo alitumia kwa mawasiliano yake na Ngowi na “washirika wake.”

Ngowi katika mawasiliano yake na Kangezi, alitumia simu zake mbili ambazo ni Na. 0713 340770 na 0754 340770.

Katika maelezo yake yaliyorekodiwa mbele ya Kamishna wa kiapo, John Malya, Kangezi anasema, amekuwa na mawaliano na maofisa usalama na viongozi ngazi ya juu katika CCM.

Njama za kutaka kumdhuru na, au kumuua Dk. Slaa zilivujishwa hadharani kwa mara ya kwanza na Mabere Marando, wakili wa mahakama kuu na mwanasheria wa chama hicho.

Alisema, chama chake kimejiridhisha kuwa mawasiliano kati ya CCM na usalama wa taifa, yamekuwa yakilenga kutoa maisha ya Dk. Slaa.

Taarifa zinasema, waliompa kazi Kangezi, walitaka kuwasilisha kwao, taarifa ya kila ambacho Dk. Slaa anatenda, ikiwamo taaarifa ya majadiliano ya vikao vya chama, pamoja na kutaja majina ya watu wanaokutana naye.

“Tarehe 28 Februari 2015, nilikuwa na Gwamaka Mwan’gonda pale Magomeni hospitali, karibu na ofisi ya mkuu wa wilaya.

Nilikutana naye hapo akiwa na gari T 213 ARS. Tuliondoka na mazungumzo yaliyokuwa ndani ya gari, ni kunishawishi kukubali kumuua Dk. Slaa,” anaeleza Kangezi.

Naye Mangula alikuwa akifanya mawasiliano na Kangezi, kupitia simu yenye Na. 0764 532222.

Kangezi anasema alikabidhiwa chupa ndogo ya kioo inayolingana na kichupa cha plastiki, ambayo aliihifadhi nyumbani kwake ili kutekeleza mauaji hayo.

Wengine ambao Kangezi amekuwa na mawasiliano mfululizo, ikiwamo kutumiwa fedha kwa njia ya simu, na ambao walikuwamo katika njama za mauaji hayo, ni Lilian Mduma na Edward Lyombe.

Lilian Mduma na Lyombe, ni wasaidizi muhimu wa Mangula. Lyombe anatumia simu tatu ambazo ni 0757 067390, 0786 873020 na 0714 280 111.

Naye Lilian, katika mawasiliano yake na Kangezi anatumia simu Na 0719 795222.

Wengine waliomo katika mpango huo, Gwamaka, Fahami Alnahdi, Dominic Gama na Vicent Shayo.

Fahani katika mkakati wake huu na Kangezi alikuwa anatumia simu Na. 0713 522222; Gama alikuwa akitumia simu mbili ambazo ni 0754 000666 na 0786 220066 na Mn’gen’ge akitumia simu tatu zenye Na. 0712 386 505, 0769 916331 na 0778 558888.

Katika maelezo yake yaliyopelekwa polisi na maofisa usalama wa Chadema, Kangezi anasema, “Mzee Philiph Mangula, nimekuwa nikiwasiliana naye kupitia simu yake Na. 0764 532222 kwa kunipigia mara kadhaa.”

Anasema, “…mzee Mangula amenitumia vocha (muda wa maongezi) mara mbili kiasi cha Sh. 50,000 (elfu hamsini). Lakini Alhamisi ya 4 Desemba mwaka jana, ndipo aliponitumia kiasi cha Sh. 150,000 (laki moja na elfu hamsini) ili nimpatie taarifa za siri za chama na kumpigia simu nikiwa katika vikao mbalimbali.”

Siku ambayo Kangezi alipokea fedha kutoka kwa Mangula, Dk. Slaa alikuwa akihudhuria kikao cha kamati kuu ya chama chake.

Kangezi anakiri pia kuwa amewahi kutoa taarifa kwa “waajiri wake” hao kuhusu nyendo za Dk. Slaa, ikiwamo katika mikutano yake na mabalozi na watu wengine mbalimbali.

Anasema, amefanya mawasiliano na Lyombe kumjulisha kuwapo kwa mkutano kati ya Dk. Slaa na mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), jijini Dar es Salaam.

Mawasiliano hayo aliyafanya saa 5:16 asubuhi. Dk. Slaa aliingia katika mkutano huo, majira ya saa tano kamili.

error: Content is protected !!