July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watumishi wa afya 900 wahitajika Kilwa

Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (kushoto) mtafiti kutoka Repoa Msami (katikati) na Kangi Lugola Mbunge wa CCM jimbo la Mwibara.

Spread the love

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilwa ina upungufu wa watumishi wa sekta ya afya 900, Bunge limeelezwa leo. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, amesema halmashauri hiyo inatakiwa kuwa na watumishi wa afya 1,275 lakini waliopo ni 375.

Ghasia amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imekuwa ikipanga watumishi wa afya moja kwa moja katika vituo vya kazi baada ya kuhitimu mafunzo yao.

Amesema changamoto kubwa iliyopo ni uhaba wa watumishi wa sekta hiyo katika soko la ajira.

Kwa mujibu wa Ghasia, katika mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha 2015/16, halmashauri imetenga nafasi mpya za ajira kwa asilimia 17 ya watumishi waliopo sasa ambayo ni sawa na idadi ya watumishi 74.

Waziri alikuwa anajibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) ambaye alitaka kujua ni hatua zipi za muda mfupi na mrefu zinachukuliwa na serikali katika kukabiliana na upungufu wa watumishi wa afya mkoa wa Lindi hususan wilaya ya Kilwa.

error: Content is protected !!