Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watumishi TRA, Polisi kizimbani tuhuma dawa za kulevya
Habari Mchanganyiko

Watumishi TRA, Polisi kizimbani tuhuma dawa za kulevya

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya
Spread the love

 

WATUMISHI watatu wa Serikali na wengine watano, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Watumishi hao ni, Askari Polisi, CPL Deodatus Leonard Massare (37), pamoja na Maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Andrew Wailes Paul (45) na Ally Juma Ally (32).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu, tarehe 19 Julai 2021 na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Kusaya amesema kuwa, watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa hizo haramu, kinyume cha Sheria ya Uhujumu Uchumi.

“Watuhumiwa wote wameshafikishwa mahakamani wakikabiliwa na makosa ya kujihusisha na usafirishaji pamoja na biashara ya dawa za kulevya, makosa ambayo ni uhujumu uchumi kwa sheria za nchi yetu,” amesema Kusaya.

Kusaya amesema kuwa, mamlaka hiyo inaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini watu waliokuwa wanashirikiana nao “pamoja na hatua hii tuliyofikia bado, tunaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waharifu wengine walioshiriki katika tukio hilo.”

Kusaya amesema watumishi hao na watuhumiwa wengine watano, walifikishwa mahakamani baada ya kukamatwa katika nyakati tofauti mkoani Dar es Salaam.

Kusaya amesema, Paul ambaye ni mtumishi wa TRA, pamoja na wenzake wawili, walikamatwa tarehe 21 Juni mwaka huu, maeneo ya Mivinjeni wilayani Temeke, Dar es Salaam, wakiwa na Heroin kilo 1.02.

Watuhumiwa waliokamatwa pamoja na Paul anayeishi Kurasini ni, Said Rashid Mgoha (45) maarufu Kindimu na George David Mwakang’ata (38), wote wakazi wa Mtoni Kijichi.

Kusaya amesema, mtumishi mwingine wa TRA, Ally, alikamatwa tarehe 23 Juni 2021, akiwa na mfanyabiashara, Abubakar Juma Abdallah, wakiwa na dawa za kulevya aina ya Methamphetamine yevye uzito wa gramu 597.61.

“Aidha, katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa Ally maeneo ya Zimbili Kinyerezi, kulipatikana pesa taslimu Sh. 82,043,000 na Dola za Marekani 5,100″. Amesema Kusaya.

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu

Amesema, Massare aliyekuwa na namba za usajili wa Jeshi la Polisi F.6763, alikamatwa tarehe 19 Juni 2021, maeneo ya Bunju Beach mkoani humo, akiwa na kilo 1.04 za dawa za kulevya aina ya Heroin.

“Tulifanikiwa kukamata askari ambaye sasa amefukuzwa kazi kutokana na taratibu za kijeshi, tulikuta nyumbani kwake dawa na bado tunaendelea kujua watu gani alikuwa anashirikiana nao katika biashara yake, tulikuta fedha Sh. 10 milioni na dola 200, alikiri za kwake,” amesema Kusaya.

Mbali na watumishi hao wa Serikali, watu wengine waliokamatwa kwa tuhuma hizo ni, wanandoa Jamal Said Nangatukile (45) na mkewe Mariyamu Rashid Bacha (28), waliokamatwa tarehe 18 Juni 2021, wakiwa na dawa hizo gramu 494.52, maeneo ya Mburahati Madoto.

“Hizo dawa tulizikuta nyumbani kwao, zikiwa zimefichwa juu ya dari, katika upekuzi tulizikuta na walikiri zilikuwa za kwao na walikuwa wanafanyabiashara hiyo,” amesema Kusaya.

Kusaya amesema, kesi za watuhumiwa hao zitatajwa mahakamani tarehe 27 Julai 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!