February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Watumishi ofisi ya Magufuli wapigwa mkwara

Kaimu Mkurugenzi wa Maadili Utumishi, Lambart Chialo

Spread the love

OFISI ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR_MUU) imeshutumu wafanyakazi katika yake kwa kukwamisha malengo ya serikali kuhusu  maadili ya watumishi kwa kuwa watoro kazin pamoja na kutumia vibaya taarifa mbalimbali za serikali , anaandika Jovina Patrick.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Maadili Utumishi, Lambart Chialo amesema misingi mikubwa ya maadili ya Utumishi wa Umma ni mingi na kwamba lazima mambo kadhaa yazingatiwe wakati wa kuyatekeleza.

Misingi hiyo ni pamoja na utaalamu, uaminifu na uwajibikaji  na kwamba changamoto kubwa zinazojitokeza katika ukuzaji wa maadili ni pamoja na utoro kazini, kutumia vibaya taarifa za serikali yaani kutoa taarifa hizo hata kwa wasiohusika nazo, matumizi mabaya ya ofisi kwa kutumia rasilimali za ofisi kwa manufaa binafsi na pia kuvaa mavazi mabaya yasiyo na maadili ya kiofisi.

error: Content is protected !!