May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watumishi 5 TRA wafariki ajalini Songwe

Spread the love

 

WATUMISHI watano Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kikosi kazi cha fast Track wamefariki dunia katika ajali ya gari eneo la Hanseketwa Oldvwawa wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songwe … (endelea).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe (RPC), Janeth Magomi amesema, ajali hiyo imetokea leo asubuhi Jumatatu, tarehe 23 Agosti 2021 wakati gari walilokuwa wamepanda T 8825 STL kugonga kwa nyuma lori T586 ANE walilokuwa wanalifukuzia.

 

RPC Janeth amesema, miili ya watumishi hao akiwemo dereva wao imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Songwe.

Waliofariki ni Azari Shifonike ambaye ni dereva, Joel Mitondwa, Saidi Buddy, Fahad Hassan na Benard Mashingi.

error: Content is protected !!