Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Watumishi 24 watunukiwa vyeti mafunzo teknolojia ya 5G
Habari Mchanganyiko

Watumishi 24 watunukiwa vyeti mafunzo teknolojia ya 5G

Spread the love

KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Zainabu Chaula amesema, jitihaza zinapaswa kufanyika ili kuhakikisha kujifunza maarafi na ujuzi wa kisasa yanayoendana na ukuaji wa sayansi na teknolojia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Chaula ametoa wito huo leo Jumatano tarehe 16 Septemba 2020 katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa watumishi 24 na wahandisi kutoka wizara hiyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL Corp.) na Tume ya Tehama.

Vyeti hivyo wametunukiwa baada ya kukamilisha mafunzo ya siku tisa ya teknolojia ya 5G yaliyotolewa na Kampuni ya Huawei Tanzania.

Dk Chaula awapongeza wahitimu wa mafunzo hayo pamoja na Kampuni ya Huawei Tanzania akisema, Serikali imedhamilia kuongeza uwekezaji kwenye nyanja ya dijitali.

“Tunahitaji kwenda na wakati na kujifunza maarifa na ujuzi wa kisasa ambao unakidhi mahitaji ya enzi hii ya dijitali na kuwa makini na mifumo ya kisasa ambayo inaweza kubadilisha au kuvuruga biashara na maisha yetu,amesema.

Jambo la muhimu zaidi tunahitaji kuimarisha ustadi wetu kwenye Tehama kupitia mafunzo na uwezeshaji mpya ili kuendana na kasi ya mabadiliko, kukabiliana na changamoto na kuwahudumia watu wetu kwa ubunifu na ufanisi,” amesema.

Katibu mkuu huyo amesema, mafunzo hayo yaliyotolewa na Huawei ni mfano mzuri wa jinsi taifa linavyoweza kufanikiwa kwa kufanya kazi na wadau binafsi wa kuaminika katika kuimarisha uwezo wake.

“Uwekezaji huu umekuja wakati mwafaka kwa kuwajengea uelewa wa kidigitali watumishi wa umma na kwa kiwango kikubwa itasaidia uboreshaji wa jukwaa la huduma za Kiserikali kidijitali, moja wapo ya vitu vitatu muhimu vya Programu ya Dijitali ya Tanzania (DTP).

Ni muhimu kwetu kukuza mazingira wazi na  mfumo wa ikolojia ambapo kila mdau anaweza kushiriki, kuchangia, na kufaidika nayo, na ambayo itasababisha ukuaji endelevu wa sekta na maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini,’’ alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania, Damon Zhang alisema tangu kuanza shughuli zake nchini mwaka 2007, imejitolea kufundisha maarifa na ustadi wa Tehama kwa Watanzania na wataalamu wote kwa kuwajengea uwezo na utaalamu wa kimataifa huku akihamasisha vijana kuanza safari ya masomo yanayohusiana na Tehama.

“Tangu tulipoanza shughuli nchini Tanzania mnamo 2007, Huawei Tanzania imejitolea kuhamisha maarifa na ustadi wa ICT kwa Watanzania na wataalamu wote kwa kuwajengea uwezo na utaalam wetu wa kimataifa na kuhamasisha vijana kuanza safari ya masomo yanayohusiana na Tehama.

Tunafikiria kwamba nchini Tanzania, watendaji wataweza zaidi kubuni maarifa ya kina yahusuyo Tehama na raia wa kawaida wataweza kuchunguza fursa na ustadi wa msingi kuhusu Tehama na vijana ambao wanapenda masomo ya Tehama wataijenga nchi yao kwenye misingi ya dijitali,”Alisema Zhang.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ditopile aungana na Wana-Kongwa kwa Iftar, wamuombea dua Rais Samia

Spread the loveKATIKA muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti...

Habari Mchanganyiko

PSSSF yawekeza kwenye viwanda 4, kuzalisha ajira 3,000

Spread the loveKATIKA kuisaidia Serikali kupunguza tatizo la uhaba wa ajira nchini,...

Habari Mchanganyiko

Luhemeja ahimiza utunzaji rasilimali maji kwa faida ya vizazi vijavyo

Spread the love  NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja...

Habari Mchanganyiko

NSSF yawapa darasa wahariri uwekezaji wa nyumba, yapewa cheti

Spread the loveMFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa wito...

error: Content is protected !!