JUMLA ya watumishi wa afya 139 wamechaguliwa kwaajili ya kupewa ufadhili wa masomo ya ubingwa na ubingwa bobezi katika fani zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Ufadhili huo umetolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya ambapo utatolewa kwa awamu na watumishi 336 watasomeshwa vyuo vya nje ya nchi huku watatu wakisomeshwa katika vyuo vya ndani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo Ijumaa tarehe 28 Oktoba 2022, wakati akitoa taarifa kuhusu mpango wa Serikali wa kuendeleza Watumishi wa Sekta ya Afya katika fani za ubingwa na ubingwa bobezi nchini.
Waziri ummy amesema, Mpango umepewa jina la “Mpango wa Samia wa kuongeza Wataalamu Bingwa na Bobezi wa Afya nchini ” utakao gharimu Sh 8 bilioni.
Aidha, Waziri Ummy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kwa kukubali kuongeza fedha kiasi hicho cha fedha zitakazotumika kugharamia wataalamu waliochaguliwa kusoma mafunzo hayo.
Leave a comment