July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Watuhumiwa wizi DCB waongezeka

Spread the love

IDADI ya watuhumiwa katika kesi ya kuiibia Benki ya Jamii ya Dar es Salaam (DCB) sasa imefika watu wanne, anaandika Faki Sosi.

Leo John Sarakikya ameunganishwa na watuhumiwa wenzake watatu waliopandishwa kizimbani mwaka jana ambao ni Manfred Sangawe (34), Suzani Kabango (32) na Belinda Chaula kwa tuhuma za kuiibia DCB jumla ya Sh. 167 milioni. Hata hivyo amekana mashitaka yake.

Kesi hiyo ilifunguliwa mwaka jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo upande wa mashitaka ni Jamhuri.

Akisomewa mashitaka yake leo na Jackson Chidunda ambaye ni mwendesha mashitika wa serikali mbele ya Huruma Shahidi, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amedai kuwa, Sarakikya na wenzake walitenda makosa hayo mwaka jana.

Chidunda amedai kuwa, watu hao kwa pamoja kati tarehe 1 na 28 Oktoba mwaka 2015 walipanga njama za kuchukua mkopa kwa njia ya udanganyifu  katika Benki ya DCB kiasi cha Sh. Mil 313.

Shitaka la pili, washitakiwa kwa pamoja kati tarehe 1 na 23 Oktoba 2015 wanadaiwa kughushi fomu ya kusafirisha fedha kiasi cha Sh. 23 Milioni iliyoonesha kuwa, muombaji ni Alphonce Hesea Nyambita kwenda kwa Hamida Arrey Khalidi ambapo ni uongo.

Shitaka la tatu mpaka la nane, yote yanahusu kughushi fomu ya kusafirisha fedha kwenda katika akaunti za watu tofauti.

Shitaka la Tisa, watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa Novemba mwaka 2015 waliibia benki hiyo  kiasi cha Sh. 29 Milioni.

Chibudi amedai kuwa, shitaka la  10 kwa watuhumiwa hao ni kuibia  benki ya DCB kiasi Sh. 27 mil ambazo walitenda kosa hilo kwa pamoja.

Shitaka la 11 lilitendwa na washitakiwa hao tarehe 6 Novemba mwaka 2015 ambapo wanadaiwa kuiibia benki hiyo Sh. 28 Milioni. Shitaka la 12  ni kuibia benki hiyo katika tarehe 9 Novemba mwaka 2015 kiasi cha Sh. 21 milioni.

Shitaka la 13 ni la watuhumiwa kutenda kosa tarehe 10 Novemba mwaka 2015 kwa kuibia benki  kiasi cha Sh. 21 milioni ambapo shitaka la 14 watuhumiwa walitenda kosa hilo tarehe 10 Novomba kwa kuibia benki hiyo Sh.19 Milion.

Hata hivyo, upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo kesi hiyo itatajwa tena tarehe 1 Agosti kwa ajili ya kusikilizwa.

Mtuhumiwa Sarakikya amepewa masharti ya dhamani ya kuwa na wadhamini wawili, mmoja asaini mali isiyo hamishika yeye thamani ya Sh 150 milioni.

error: Content is protected !!