Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Watuhumiwa watatu ujambazi wauawa Dar
Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa watatu ujambazi wauawa Dar

Spread the love

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam nchini Tanzania, limewaua watuhumiwa watatu wa ujambazi eneo la Chamazi, waliokuwa kwenye gari aina ya Nissan X Trail lenye namba za usajili T 855 ATE waliotaka kufanya uhalifu katika kituo cha kuuzia mafuta. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Tukio hilo lilitokea tarehe 26 Julai, 2020 saa 2 usiku ambapo majambazi hao walikuwa na siraha mbili ambazo ni Sort gun na Bastora ndogo pamoja na sare za jeshi la polisi.

Majambazi hao waliuwawa baada ya kurushiana risasi na polisi ambapo watatu walifariki hapo hapo huku mmoja akifanikiwa kukimbia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi tarehe 30 Julai 2020, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema, mara baada ya tukio hilo polisi walikagua gari hilo na kukuta siraha hizo sambamba na pingu na kamba aina na katani.

“Askari baada ya mashambulizi yale walifanya upekuzi kwenye gali lile na kufanikiwa kupata sare za polisi na pingu moja.”

“Lakini, pia walifanikiwa kupata radio call moja sambamba na hizo siraha nilizozitaja na ndani ya gari hiyo ilipatikana Pleti namba ya gari yenye namba za usajili T 832 DCW. Alisema Kamanda huyo,” amesema Mambosasa

Mambosasa amesema, baada ya uchunguzi pleti namba iliyopatikana ndani ya gari hiyo, ndio namba halisi ya gari hiyo ilikuwa inatumika kwenye ujambazi huo.

Kabla ya tukio hilo, majambazi hao walimkamata Salehe Masoud Jani ambaye ni wakala huku wakiwa wamevalia sare za jeshi la polisi na kuhamisha kiasi cha Sh. 19 milioni zilizokuwa kwenye simu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!