March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Watuhumiwa wa mauaji ya Dk. Mvungi waachiwa, wakamatwa

Spread the love

WATUHUMIWA wa maauji ya Dk. Sengodo Mvungi aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameachiwa huru na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada Serikali kuomba kuondolewa kwa shitaka hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Watuhumiwa hao sita wameachiwa huru leo baada ya mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuomba kuondolewa kwa shitaka hilo na kwamba hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Watuhumiwa hao ni pamoja na Msigwa Matonya, Mianda Mlewa, Paulo Mdonondo, Longishu Losindo, Juma Kangungu na John Mayunga.

Wakili mkuu wa serikali Nasoro Katuga, aliwasilisha maombi hayo na mahakama ikakubali kuwaachia washtakiwa hao huru.

Baada ya kuachiwa huru walikamatwa tena na kupelekwa Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka mapya ya mauji ya Dk. Mvungi.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo la mauaji ya kukusudia siku ya jumapili terehe 3 Novemba mwaka 2013, eneo Msakuzi Mbezi jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!