July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Watuhumiwa dawa za kulevywa waomba kutupwa baharini

Spread the love

RAIA watatu wa Pakistani na wanane wa Iran wanaokabiliwa na kesi ya kuingiza nchini dawa za kulevya, wameiomba Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam iwatupe baharini, anaandika Faki Sosi.

Watuhumiwa hao wamemwomba Warialwende Lema, Hakimu Mkazi Kisutu watupwe baharini kutoka na hali ngumu wanayokutana nayo gerezani na kwamba, hawana ndugu hapa nchini.

Watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 4 Februari, 2014 wakiwa na dawa za kulevya aina Heroin kilo 200.5 zenye thamani ya Sh. 9.02 bilioni wakiziingiza nchini kupitia Bahari ya Hindi.

Watuhumiwa hao wakati wanakamatwa walikuwa 12 ambapo wamebaki 11 kutokana na mmoja kati yao kufariki dunia. Aliyefariki ni Kapteni Ayoub Mohamed.

Wanaoendelea na kesi hiyo ni Buksh Mohamed, Fahiz Dauda, Khalid Ally, Abdul Somad, Saeed Sahury, Bashir Afraz, Morad Gwaram na Hazir Azad Rais wa Iran.

Raia wa Pakistani ni Buksh Mohamed, Rahim Baksh na Abdul Bakashi ambapo kesi hiyo imeghairishwa hadi tarehe 4 Aprili mwaka huu.

error: Content is protected !!