
Watu weusi wana uwezekano mkubwa wa kujisikia upweke kuliko watu wengine kwa ujumla, kwa mujibu wa utafiti mpya. BBC imeripoti … (endelea).
Takwimu kutoka kwa Taasisi ya masuala ya Afya ya Akili (Mental Health Foundation) zinaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya watatu weusi amewahi kukumbwa na hisia za upweke.
Hiyo inalinganishwa na idadi ya watu kwa ujumla ambapo mtu mmoja kati ya wanne alikuwa ameripoti upweke wakati fulani wa maisha yake au wakati wote.
Mmoja kati ya watu watatu wenye umri wa miaka 16-24 pia walisema wanapata upweke.
Msemaji wa taasisi hiyo anasema ubaguzi wa rangi na usawa wa kijamii vinaweza kuchangia viwango hivi vya juu.
Taasisi hiyo ilichunguza watu 6,000 kote Uingereza.
Huu upweke unatokana na ubaguzi wa rangi. Hivyo, hii tafiti haina maana kama haisemi mazingira yanayosababisha upweke.
Lengo la tafiti ni kuwadhalilisha watu weusi wa Ulaya.