March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Watu ‘wasiojulikana’ wazidi kuinyanyasa Chadema

Dady Igogo, Diwani wa Gangalonga ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa wa Iringa

Spread the love

NAIBU Meya wa Manispaa ya Iringa ambaye ni Diwani wa Kata ya Gangalonga (Chadema), mkoani Iringa Dady Igogo, amenusururika kuwa baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Igogo ameeleza kuwa ametishwa kutokana na mfululizo wa matukio hayo amedai kuwa ni kiashiria kibaya cha amani.

Anasema kuwa amesikitishwa na kitendo hicho kutokana kuwa kinaviashiria vya ubaguzi wa kisiasa ambapo ameeleza kuwa alivamiwa na vijana wenye pikipiki ambapo walimshambulia.

“Wakati narudi nyumbani nilisimamishwa na pikipiki kama nne waliokuwa kama wanataka kuniuliza jambo. Nilifungua kioo! Ghafla walinivamia na kuanza kunipiga na kunitoa kwenye gari. Niliacha gari na kufanikiwa kukimbia kwa miguu.

“Walichukua simu yangu, pamoja na kuchomoa ufunguo wa gari wakaondoka. Wakati wananipiga walikuwa wanasema ‘kahamishe makaburi ya kwenu’,” ameeleza Igogo.

Amesema kuwa amesikitishwa pia baada ya kuuwawa kwa kiongozi wa Chadema Kata ya Hananasif Daniel John. “Inaumiza sana. Sijui Mama yake Ben Saanane yuko katika hali gani?”

Ameeleza kuwa kuendelea kuwa mwanasiasa wa upinzani ni hatari ambapo hata baadhi watendaji wamekuwa vinara wa kufanya ubaguzi wa kisiasa nchi akimtolea mfano Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ametoa tamko la wazi kuwa anawabagua wapinzani.

Habari ambazo hazitathibitishwa zinadai kuwa Igogo amejiuzuru nafasi yake ya Unaibu Meya wa Manispaa ya Iringa, sababu za kujizuru kwake hazijafahamika.

error: Content is protected !!