Thursday , 29 February 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Watu wasiojulikana’ wapiga hodi polisi
Habari Mchanganyiko

‘Watu wasiojulikana’ wapiga hodi polisi

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
Spread the love

JESHI la Polisi Kanda ya Maalumu ya Dar es Salaam limeanza kufanya msako kuwasaka watu waliofanya mauaji ya askari polisi aliyeokotwa juzi akiwa amefariki, anaandika Angel Willium.

Askari Charles Yanga mwenye namba X-G 475 hivi karibuni akiwa amefariki pembeni ya uzio wa kambi ya polisi Ukonga na mwili wake ulionekana kuwa na majeraha kwenye paji la uso huku sikio moja likiwa limekatwa.

Katika kufuatilia polisi wamegundua askari huyo ameuwawa na watu wasiyojulikana kisha kutelekezwa katika maeneo ya kambi ya polisi.

Aidha, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ameagiza kuchukuliwa hatua askari wanaodaiwa kuwapiga wananchi katika eneo la Gogo la Mboto jijini Dar es Salaam kwa madai ya kulipiza kisasi.

“Kama Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, jambo ambalo limefanyika kwa siku tatu hizo halikubaliki na kama kuna matatizo ya askari na raia kulikuwa kuna eneo la kupeleka matatizo hayo.”

Mnamo tarehe 21 mwezi wa 10 mwaka 2017 majira ya saa 06:00 huko maeneo ya kambi ya polisi Ukonga jijini Dar es Salaam makao makuu mkoa wa kipolisi, askari walikuta mwili wa polisi nje ya kambi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!