March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Watu wasiojulikana’ wamuibua  Mkuu wa Majeshi

Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania. Picha ndogo ni muonekano ya watu wasiojulikana

Spread the love

SAKATA la uvamizi na kupigwa risasi na watu wasiojulikana limemuibua Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Venance Mabeyo ambaye amesema vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wa matukio hayo, anaandika Mwandishi Wetu.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio mabaya ya uhalifu likiwamo la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema),  ambaye amepigwa risasi zaidi ya 30  akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.

Tukio lingine ni lile la kupigwa risasi, Meja Jenerali mstaafu, Vincent Mribata akiwa nyumbani kwake jambo ambalo limemuibua Jenerali Mabeyo na kutoa kauli nzito.

Amesema watawasaka watu hao na watawakamata wote wanaohusika na vitendo hivyo  vya uhalifu na kuwaomba wananchi kuviachia vyombo vya dola vifanye kazi yao ili vitoe majibu.

error: Content is protected !!