February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Watu 60 mbaroni kwa kuharibu miundombinu ya Tanesco

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa

Spread the love

ZAIDI ya watu 60 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za uharibifu wa miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 2 Oktoba 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na wanahabari.

Kamanda Mambosasa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika nyakati tofauti kwenye operesheni za kusaka waharibifu wa miundombinu ya shirika hilo, zinazoendeshwa na TANESCO kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Sambamba na watuhumiwa hao, Kamanda Mambosasa amesema Jeshi la Polisi linamshikilia dereva bodaboda mmoja anayefahamika kwa jina la Matthew Joseph kwa kosa la kumiliki na kuitumia katika matukio ya kihalifu, bunduki aina ya shotgun.

Amesema watuhumiwa hao wanaendelea na mahojiano na kwamba yakikamilika watachukuliwa hatua za kisheria zaidi.

error: Content is protected !!