July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watu 298 wafariki kwa ajali Dodoma

Spread the love

JUMLA ya watu 298 wamepoteza maisha katika ajali 233 za barabarani zilizotokea katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2015 mkoani Dodoma. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Katika ajali hizo ambazo pia ziliwajeruhi vibaya watu wapatao 680, huku jumla ya wanaume 251 walifariki dunia na idadi ya wanawake walioukufa katika ajali hizo ni 47.

Akizungumza na MwanaHALISI Online jana ofisini kwake, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Dodoma, Nuru Selemani amesema chazo kikubwa cha ajili hizo ni matumizi ya pombe miongoni mwa madereva.

“Ajali nyingi zimesababishwa na madereva ambao walithibitika kuwa wametumia pombe na aina nyingine za madawa ya kulevya,” alieleza.

Hata hivyo alizitaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na uchakavu wa barabara pamoja na uelewa mdogo wa matumizi ya barabara miongoni mwa waenda kwa miguu.

Akiongea juu ya juhudi zinazofanywa na jeshi hilo katika kupambana na wimbi la ajali barabarani, Kamanda Selemani amesema wanaendelea na program mbalimbali za kutoa elimu ya matumizi mazuri ya barabara, pamoja na semina mbalimbali kwa madereva wa magari na bodaboda.

“Katika kipindi cha mwaka jana tuliwakamata madereva 2,147 kwa ajili ya makosa mbalimbali ya matumizi mabaya ya barabara, wakati mwaka huu tumeweza mpaka sasa kuwakamata madereva wapatao 4,012,” alieleza.

error: Content is protected !!