Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Watu 275 wakamatwa tuhuma za mauaji
Habari Mchanganyiko

Watu 275 wakamatwa tuhuma za mauaji

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime
Spread the love

 

JESHI la Polisi nchini Tanzania, linawashikilia watu 275 kwa tuhuma za mauaji, yaliyotokea nchi nzima kuanzia Mei hadi Julai 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana tarehe 20 Julai 2021 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP, David Misime, akieleza tathmini ya operesheni endelevu ya jeshi hilo katika kusaka wahalifu nchi nzima.

“Waliokamatwa kujihusisha na mauaji ni 275, kati yao waliokamatwa kutokana na mauji ya wivu wa kimapenzi ni 21, imani za kishirikina ni 22 na 231 kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa pamoja na kujitafutia kipato kwa njia za kiuhalifu,” amesema Kamanda Misime.

Akielezea tathmini ya operesheni hiyo, Kamanda Misime amesema watuhumiwa 5,429, walikamatwa kufuatia zoezi hilo.

Amesema, 63 walikamatwa kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha, 141 wakikamatwa kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia nguvu. Huku 1,265 walikamatwa kwa tuhuma za kuvunja nyumba na kuiba.

Kamanda Misime amesema, waliokamatwa kwa makosa ya kubaka ni 508,  wakati 125 wakikamatwa kwa tuhuma za kulawiti.

Kufuatia operesheni hiyo, watu 2,300 walikamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

“Dawa za kulevya aina ya Heroin kiasi cha kilo 540 kilikamatwa, Cocain gramu 104, bhangi kilo 3304.321 zilikamatwa. Mashamba ya bhangi hekari 11.75 ziliharibiwa. Mirungi kilo 2233.394 zilikamatwa,” amesema Kamanda Misime.

Msemaji huyo wa Jeshi la Polisi amesema, watu 398 walikamatwa kwa tuhuma za kutengeneza pombe haramu ya gongo na kuuza, kiasi kilichokamatwa ni lita 13612.175 na mitambo ya kutengeneza pombe hiyo iliyokamatwa ni 94.

“Waganga wa ramri chonganishi waliokamatwa ni 15. Aidha katika watuhumiwa wote 5,429 waliokamatwa kulingana na ushahidi ulivyowagusa, wameshafikishwa mahakamani,” amesema Kamanda Misime.

Kamanda Misime amewataka wananchi wajiepushe na vitendo vya uhalifu.

“Jeshi katika kila mkoa na kikosi limejipanga vizuri kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inakuwa shwari. Tunatoa wito na karipio kali kwa wahalifu kuachana na vitendo vya kiuhalifu na pia wale wote wanaoendelea kushawishi wananchi kwenye vitendo vya ukiukwaji wa sheria za nchi,” amesema Kamanda Misime.

“Silaha zilizokamatwa katika operesheni hiyo ni 37, ikiwemo bastola nne, shortgun tatu, magobore 29 na uzigun moja,” amesema Kamanda Misime.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa vya ujenzi, samani kwa shule ya msingi Sinyaulime, Chuo cha FDC Morogoro

Spread the loveBENKI ya NMB imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa shule ya...

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

error: Content is protected !!