Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Watu 20 wafa ajalini, Rais Samia atoa pole
Tangulizi

Watu 20 wafa ajalini, Rais Samia atoa pole

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa familia za watu 20 waliofariki ajalini na wengine 15 kujeruhiwa. Anaripoti Erick Mbawala, TUDARco … (endelea).

Ajali hiyo iliyotokea jana Jumatatu tarehe 8 Agosti saa 4.00 usiku katika eneo la Mwakata barabara ya Isaka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasilinao ya Rais Ikulu, Rais Samia amevitaka vyombo vyote vinavyohusiaka na ausalama barabarani kuongeza juhudi za kudhibiti ajali.

Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria aina ya Toyota HIACE yenye namba za usajili T350 BDX, gari ndogo aina ya IST yenye namba za usajili T880 DUE, lori pamoja na Trekta.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo imeelezwa kuwa Toyota HIACE, iligongana uso kwa uso na Lori yenye namba za usajili T 658 DUW na kusababisa ajali kwa magari mengine mawili yaliyokuwa yakipita eneo hilo pia.

Taarifa zimeeleza kuwa watu 17, walipoteza maisha papo hapo na wengine watatu walifariki baada ya kufikishwa katika kituo cha Afya, pia taarifa imeripoti majeruhi 15 ambao bado wanapata matibabu wakiwa chini ya uangalizi wa hospitali ya Kahama katika Mkoa huo.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Kahama, DK. Deogratius Nyanga, imethibitisha kupokea miili ya watu 20 na majeruhi 15.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP. Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa dereva wa Trekta amekimbia na juhudi za kumtafuta zinaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!