Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watu 175 wapata msaada wa kisheria LSF
Habari Mchanganyiko

Watu 175 wapata msaada wa kisheria LSF

Spread the love

WATU takribani 175 wamepatiwa huduma ya msaada wa kisheria na Shirika la Services Facility (LSF), katika wiki ya Sheria iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 22 hadi 29 Januari 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza wakati wa kuhitimishwa wiki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala amesema shirika hilo kupitia wasaidizi wake wa kisheria limeweza kushughulikia mashauri mbalimbali ikiwemo migogoro ya ndoa, matunzo ya watoto, mirathi pamoja na migogoro ya ardhi.

Lulu amesema kuwa, LSF imekuwa ikishirikiana na mahakama kwa ajili ya kukuza upatikanaji wa haki nchini Tanzania kwa kuwasaidia wananchi kupata haki zao.

“Wiki ya Sheria imekuwa muhimu kwetu kama wadau wa mahakama kwani kupitia wasaidizi wa kisheria tumeweza kutoa huduma bure kwa wananchi waliotembelea banda letu kwa njia ya usuluhishi. Kupitia wiki hii tumesaidia watu 175 ambapo wanaume ni 73 na wanawake ni 102,” amesema Lulu.

Naye msuluhishi kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Usuluhishi, Jaji Dk. Zainab Diwa Mango, amesema kwa sasa  mahakama zinakabiliwa na mashauri mengi yanayoendelea, ambayo pia yanahitaji ushahidi ili kufanya uamuzi wa mwisho, jambo ambalo hulazimika kuchukua muda mrefu tofauti na kutumia njia ya usuluhishi.

“Usuluhishi hauchukui muda mrefu, unachukua muda wa siku 30 tu. Hii ni kwa mujibu wa katiba yetu Ibala ya 107A(1)(d), ambayo inasisitiza kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika mgogoro,” ameeleza Dk. Mango.

Dk. Mango anaendelea kueleza kuwa usuluhishi unapunguza muda mwingi mahakamani na kumpa muda mteja muda wa kufanya shughuli za kiuchumi, kwa kuwa katika usuluhishi hakuna dhana ya kila mtu kutaka kushinda, kitu ambacho huleta changamoto kubwa kwenye mashauri yanayoendeshwa mahakamani.

“Kituo chetu cha usuluhishi kilianza mwaka 2015 na mwaka huu tumetoa taarifa maalum ya utekeleza wa shughuli zetu kwa kipindi cha miaka saba. Kupitia kauli mbiu ya mwaka huu itasaidia kuonesha umuhimu wa usuluhishi kwa wananchi,” amesema Dk. Mango.

Baadhi ya wananchi waliofika na kunufaika na huduma za usuluhishi katika maadhimisho ya wiki ya sheria wamesema jamii imekuwa na changamoto nyingi za kisheria lakini upatikanaji wa haki umekuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya kesi zinazofikishwa mahakamani ili kupata ufumbuzi.

Joyce Massawe amesema na mgogoro wa mtoto kati yake na ndugu wa marehemu mume wake, ambao walimnyang’anya bila kufuata utaratibu, lakini maadhimisho ya wiki ya sheria yamesaidia kuweza kupata suluhu nzuri kati yake na ndugu wa marehemu mumewe baada ya kuitwa ili kufanya usuluhishi.

Filbert Swabi ameshukuru uwepo wa wiki ya sheria, ambapo ameweza kupata suluhu kati yake na mkewe Deborah Ernest, baada ya kuwa mgogoro wa ndoa kwa kipindi kirefu bila kupata utatuzi wa kudumu.

Akiongea kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria wengine wanaofadhiliwa na LSF, Anthony Isakwi amesema kuwa wasaidizi wa kisheria wamekuwa wakifanya kazi ya kutatua changamoto mbalimbali katika jamii kwa kutoa hudma za msaada wa kisheria na elimu ya kisheria, ambapo usulushishi umekuwa ukitawala zaidi ili kupata ufumbuzi katika migogoro.

“Usuluhishi imekuwa mbinu yetu kubwa tunayoitumia katika kutatua kesi mbalimbali zinazoripotiwa kwetu.  Usuluhishi umekuwa unafanyika zaidi kwenye kesi za madai. Lakini kesi za jinai kama vile ukatili wa kijinsia na kadhalika tunashirikiana na wadau wengine kama vile Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), ambao hupeleka shauri mbele zaidi kwenye vyombo vya utoaji haki ikiwemo mahakama,” amesema  Isakwi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!