October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watu 150 wahofiwa kufa ziwani

Ziwa Kivu

Spread the love

WATU 150 wanahofiwa kufa baada ya boti walilokuwa wanasafiria kuzama kwenye Ziwa Kivu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa ya tukio hilo imethibitishwa na Rais wa Congo-DRC, Felix Tshisekedi jana terehe 16 Aprili 2019 kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter.

Katika andiko lake hilo, Rais Tshisekedi alitoa salamu za pole huku akielezwa kusikitishwa kwake na mkasa huo.

Gavana wa Mkoa wa Mashambani wa Tshupa Kaskazini mwa Congo alinukuliwa na vyombo vya habari akisema tukio hilo limetokea katika Ziwa Kivu karibu na eneo la Kalehe  jioni ya Jumatatu tarehe 15 Aprili 2019.

 Kwa mujibu wa taarifa ya za vyombo vya habari nchini Congo-DRC, miili ya watu watatu imeopolewa, na manusura 33 katia kadhia hiyo imeokolewa.

error: Content is protected !!