November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watu 1,000 waugua Dengue Dar

Mbu wanaambukiza ugonjwa wa Dengue

Spread the love

WATU takribani 1,000 wameugua ugonjwa wa Dengue Jijini Dar es Salaam kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Mei 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo amesema Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Yudas  Ndungile leo tarehe 11 Mei 2019 wakati akizungumza na kituo moja cha redio  hapa nchini.

Dk. Ndungile amesema ugonjwa wa Dengue kasi yake ya kusambaa jijini Dar es Salaam imeongezeka, na kuwataka wakazi wa jiji hilo kuchukua tahadhari.

Aidha, ametaja sehemu zinazo ongoza kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Dengue ikiwemo Wilaya ya Ubungo, Kinondoni na Ilala.

Amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kusafisha mazingira yanayo wazunguka ili kuondoa mazalia ya mbu wanaoeneza ugonjwa wa Dengue.

Dk. Ndungule amewataka Wananchi kufika hospitalini na katika vituo vya afya mapema pindi wanapo ona mabadiliko ya afya zao, ili wafanyiwe uchunguzi wa kitabibu, huku akisisitiza kwamba ugonjwa huo unapimwa bure.

error: Content is protected !!