August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watu 10 wafariki wakiwemo wanafunzi wanane ajali basi la shule

Spread the love

 

WATU 10 ikiwemo wanafunzi wanane, wamefariki dunia huku 17 wakijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Mji Mwema, mkoani Mtwara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Taarifa ya ajali hiyo iliyotokea mapema leo Jumanne, tarehe 26 Julai 2022, imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mtwara, ACP Nicodemus Katembo, akizungumza na wanahabari.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Katembo, watoto watano kati ya majeruhi 17, wako katika chumba cha uangalizi maalum (ICU), huku wengine wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula.

Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni kufeli kwa mfumo wa breki wa gari lililokuwa limebeba wanafunzi hao kutoka Shule ya Msingi ya King David na wa shule jirani.

Akizungumzia ajali hiyo, Mkuu wa Shule ya Msingi ya King David, amesema kati ya wanafunzi wanane waliofariki dunia, watano ni wanafunzi wa shule yake pamoja na dereva.

error: Content is protected !!