January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watoto wenye Saratani wasaidiwa

Mkurugenzi wa Tiba shirikishi Muhimbili, Dk. Praxede Ogweyo akikabidhi msaada wa watoto wenye saratani

Spread the love

JUMUIYA ya wauguzi Tanzania, imetoa msaada wa dawa, vifaa vya shule na vya kuchezea kwa watoto wanaondelea kupata matibabu ya Saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili vyenye dhamani ya shilingi 2,250,000. Anaandika Sarafina Lidwino…(endelea)

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Tiba shirikishi Muhimbili, Dk. Praxede Ogweyo, amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo kutokana na baadhi ya wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwahudumia.

Ogweyo ameeleza kuwa, kuna baadhi ya watoto wanatoka nje ya mkoa, wanakuja kwa ajiri ya matibabu, hivyo hukaa kwa muda mrefu hospitalini hapo hadi pale watakapo pona.

“Kuna watoto wengine wanakaa miezi 6 hadi 8 wakiwa bado wapo hospitalini hapa, hivyo ili kuonyesha kuwa tunawajali na kuwapenda, tunajitolea kuwatafutia waalimu ambao wamebobea ili waendelee kuwafundisha kwa muda wote wanaokuwepo ili wasipoteze mwelekeo wa masomo yao,” amesema Ogweyo.

Mmoja wa wauguzi wa watoto hao, Kulwa Kaombwe, amelieleza MwanaHalisiOnline kuwa yeye pia ni mmoja kati ya watu wanaoguswa sana na tatizo hilo la ugonjwa wa saratani kwa watoto.

Kaombwe amesema, licha ya kutoa muda wake kuwasaidia watoto hao, bado kuna changamoto kubwa ambazo wanakutana nazo, hivyo wanahitaji msaada zaidi.

“Licha ya Serikali kutangaza kuwa matibabu ya sarataini ni bure, lakini bado kuna changamoto ya kucheleweshwa kwa dawa, hazifiki muda muafaka, hivyo kusababisha ugonjwa kuongezeka,” amesema Kaombwe.

Aidha, Kaombwe ameeleza kuwa, idadi ya wagonjwa hospitalini hapo ni kubwa, takribani watoto 500, ambao wana saratani ya aina tofauti ila iliyoshamiri sana ni ya macho na damu.

error: Content is protected !!