August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watoto 11,499 watendewa ukatili 2021

Dk. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Spread the love

 

WAZIRI wa Maendeleo ya jamii, Dk. Doroth Gwajima amesema jumla ya watoto 11,499 wamefanyiwa ukatili mwaka jana. Kati yao 5,899 walibakwa na walilawitiwa ni 1,114.

Amesema kwa wastani wa watoto 140 kwa mwezi hutendewa ukatili ilihali kati yao 93 hutendewa vitendo vya ulawitiwa 93 kila mwezi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam  … (endelea).

Dk. Gwajima ametoa kauli hiyo leo tarehe 30 Julai, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vipaumbele vya wizara hiyo kuelekea mwaka 2022/2023.

Amesema vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kama vile ubakaji, mimba za utotoni, ukeketeaji na ulawiti vimeendelea kuongezeka.

Amesema hali hiyo inasababishwa na mwamko mdogo wa waathiriwa kuripoti matukio hayo kwani takwimu zinaonesha ni asilimia 12 ndio wanaoripoti matukio hayo kwenye vyombo vya dola huku wengine wakibaki nayo nyumbani kwa madai ya kumaliza kindugu.

“Asilimia 60 ya matukio haya yanatokea nyumbani waliko ndugu na wazazi na asilimia 40 shuleni, hivyo ukatili huu kwa watoto unasababisha athari nyingi ikiwamo mtoto kupata maradhi na huenda pia akageuka kuwa mkatili kwa watu wazima ndio maana hili tutalifanyia kazi kwa nguvu,” amesema.

Aidha, amesema majukwaa ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa watoto ndani na nje ya shule yataanzishwa katika ngazi za shule za msingi na sekondari.

Amesema Serikali imeandaa muongozo wa taifa wa uundaji wa uendeshaji wa mabaraza ya watoto Tanzania pamoja na muongozo wa taifa wa dawati la ulinzi na usalama wa mtoto ndani na nje ya shule ambayo yote ilizindulia katika siku ya mtoto wa Afrika.

Amesema katika kutekeleza malengo ya miongozo hiyo, zaidi ya Sh milioni 386.7 zitatumika katika utoaji wa elimu kwa watoto, wazazi na walimu kuhusu athari za ukatili wa watoto.

Kuhusu ukatili wa watoto mitandao ambao sasa umeshika kasi kutokana na ukuaji wa teknolojia ya habari na maawasiliano, Waziri Gwajima amesema Serikali imeunda kikosi kazi cha taifa cha ulinzi na usalama wa mtoto mtandaoni chenye lengo la kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya ukatili wa mtandaoni na kuwasaidia kutumia vifaa vya kielektroniki kwa usahihi na usalama.

“Pia kikosi kazi kitakuwa na jukumu la kuratibu wadau katia serika na sekta binafsi kuhuisha masuala ya ukatili dhidi ya watoto mtandaoni na utekelezaji wa sheria ya makosa ya mtandao mwaa 2015 na sheria yam toto ya mwaka 2009,” aemsema.

Ameongoza kuwa Serikali imetenga kiasi cha Sh milioni 177.9 katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 zitakazotumika kutoa elimu kwa watoto, wazazi na walimu kuhusu athari za ukatili wa watoto mtandaoni.

Pia imeandaa machapisho majarida ya kufundisha watoto na wazazi na walimu kuhusu ukatili wa watoto mtandaoni sh milioni 177.9 zimetengwa kusukuma ajenda hiyo.

error: Content is protected !!