November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watoa huduma za afya ‘wanaolala’ wikiendi kikaangoni

Prof, Abel Makubi Mganga mkuu wa Serikali

Spread the love

WIZARA ya Afya imeanzisha kamati za kusimamia uadilifu ili kupunguza malalamiko ya wateja kwenye Hospitali ya Taifa, Hospitali Maalumu, hospitali za rufaa, za kanda na hospitali za rufaa za mikoa.

Hatua hiyo imekuja baada ya wizara hiyo kuchambua maoni ya wananchi katika utekelezaji wa sera ya afya kupitia ‘ Afya maoni center’  ambapo wananchi wengi walilalamikia utoaji huduma usioridhisha katika hospitali hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Maoni hayo yalitolewa kwa njia maongezi ya simu, ujumbe mfupi (sms), vyombo vya habari, ana kwa ana na mitandao ya kijamii katika kipindi cha kuanzia tarehe 25 Februari hadi 14 Agosti, 2022.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 26 Septemba, 2022 na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi imesema katika malalamiko 230 waliyopokea imeonesha kuwa maoni mengi hupokewa siku ya Ijumaa hivyo kuonesha kuwa ufanisi wa huduma za afya huoungua katika siku za mwishoni mwa wiki.

“Malalamiko yanayoongoza yanatokana na huduma za tiba ikifuatiwa na huduma za chanjo,” amesema.

Amesema kutokana na hali hiyo, mbali na kuundwa kwa kamati ya kusimamia uadilifu, pia wameundsa mpango wa kutoa mafunzo endele kwa watumishi ili kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa.

“Pia kuwachukulia hatua watumishi wote wanaokiuka taratibu za utumishi wa umma na mwisho kuhakikisha kunakuwapo na uwazi katika gharama za matibabu na utaratibu wa kuoata huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya,” amesema na kuongeza;

“Wizara inapenda kuwasihi wananchi kuendelea kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwa namba 199 na 0673050000 endapo watakuwa na malalamiko, kero, ushauri na pongezi kuhusu huduma za afya zinazvyotolewa katika hospitali hizo.

error: Content is protected !!