October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watia nia wafutiwa mishahara

Spread the love

SERIKALI imeagiza kwamba, watumishi wa umma waliotia nia ya kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa, wasilipwe mishahara yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Barua hiyo imetolewa na Ofisi ya Msajili wa Hazina tarehe 21 Julai 2020, likiwataka wakurugenzi na wakuu wote wa taasisi kuhakikisha, watumishi hao hawalipwi mishahara hiyo kuanzia Julai 2020.   

Neema Msonda, Msajili wa Hazina pia amewataka wakuu wa taasisi hizo kuandaa na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maelekezo hayo ifikapo tarehe 25 Julai 2020.

“Maelekezo haya ya kutolipa mshahara wa mwezi Julai, yanawahusu watumishi waliopatiwa vibali/ruhusa na waajiri wao pamoja na watumishi waliogombea bila vibali kutoka kwa waajiri wao au kupitia mamlaka stahiki,” imeeleza barua hiyo.

error: Content is protected !!