Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Watendaji Kata wapewa rungu katika maeneo yao
Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata wapewa rungu katika maeneo yao

Spread the love
MKUU wa Wilaya ya Kilosa, Morogoro, Adam Mgowi amewataka watendaji wa kata kufanya kazi ya kusimamia mambo yanayotolewa na Serikali ikiwemo rasilimali fedha, mali, watu na kuhakikisha kila jambo linatimia kwa wakati uliopangwa mambo yatakayosaidia upatikanaji wa elimu bora wilayani humo. Anaripoti Christina Haule, Kilosa … (endelea).

Akifungua kikao cha watendaji wa Wilaya kilichoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kuelimisha jamii lijulikanalo kama Dira lililoendesha mradi elimu unaofadhili na The Foundation For Civil Society (FCS), mkuu huyo wa wilaya alisema, mojawapo ya jambo kubwa walilokabidhiwa ni usimamizi wa rasilimali za Umma zinazotolewa kwa ajili ya kuhakikisha elimu bora inapatikana na watoto na kuona wanafanikiwa kiwilaya na hatimaye kimkoa.

Mkuu huyo wa Wilaya aliwaasa viongozi waliopo kwenye ngazi za vijiji, kata na wilaya kushirikiana na watendaji wa kata na kuhakikisha Serikali, walimu na wazazi wanafanya kazi vyema yenye kuleta mafanikio kwenye sekta ya elimu.

Hata hivyo aliishukuru Dira kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuiunga mkono Serikali, moja ya ahadi zake kwa wananchi ni kutoa elimu bora na bure kwa kwamba watoto wote wa kitanzania.

Alisema, Mpango waliokuja nao Dira wa kuwasaidia kuhamasisha au kuwajengea uwezo wa namna gani ya kuweza kusimamia kazi za Serikali utazidi kuwasaidia licha ya kuwa kazi ya kwanza kubwa imeshafanywa na mheshmiwa Rais John Magufuli ya kuwasaidia watoto wote wapate pesa ya kuweza kwenda shule na kusiwe na changamoto ya pesa.

“Ni kweli serikal inatoa pesa, lakini pesa pekee haiwezi zikasaidia lolote kama hakutakuwa na usimamizi thabiti na madhubuti kutoka kwetu sisi tuliopewa jukumu la kusimamia maendeleo,” alisema Mgowi.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka watendaji hao wa kata kuhakikisha wanasimamia rasilimali za Umma ikiwemo madawati shule na kuona yanakuwa kwenye ubora muda mrefu tofauti na ilivyo kwa sasa madawati hutengenezwa na kuharibika mapema kwa kukosa uangalizi.

“Jukumu kubwa anapaswa kufanya nani kama sio wao watendaji wa kata ambao wanafanya juhudi kwenye mambo mbalimbali mfano utengenezaji wa madawati usimamizi wake umekuwa mbovu, ukifika shuleni ukiuliza, robo yatakuwa yamepotea na ikifika baada ya miaka mitano nusu yatakuwa hayapo kabisa, ni wajibu wenu kwenda kusimamia hayo, na kwamba haya yote ndio mmejengewa uwezo na Dira, hivyo wajitambue,” alihoji Mgowi.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alizungumzia suala la elimu duni wilayani humo na kuweka wazi kuwa wapo baadhi ya wazazi ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha elimu kufuatia kuwakataza watoto wao wasisome zaidi na kufaulu ambapo aliwataka kuondokana na mitazamo potofu itayosaidia kuinua kiwango cha taaluma.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mwambambale Asajile Lukas aliishukuru Dira kwa kuendelea kutoa elimu kwenye sekta ya elimu wilayani humo na kusema kuwa Dira wamekuwa wakitoa elimu ya PETS katika sekta ya elimu upande wa sekondari na wameona manufaa yake na kwamba wanategemea matokeo mazuri pia katika elimu ya msingi.

Akizungumza kuhusu mradi huo Mkurugenzi wa Dira, Erasmo Tullo, alisema Mradi huu wa Wajibu wa jamii na viongozi katika kufuatilia na kusimamia matumizi ya rasilimali za umma (PETS) kwa Lengo la kuimarisha Uwazi, Ushirikishwaji na Uwajibikaji miongoni mwa Viongozi na Jamii ili Kuongeza ufanisi katika Usimamizi wa Rasilimali za Umma Sekta ya Elimu.

Tullo alisema, rasilimali za Umma zinapaswa kuweza kutumika vizuri katika kuboresha Miundombinu ya Elimu ikiwemo Vyumba vya Madarasa, Maabara, Vyumba vya kubadilishia Taulo(Pedi) watoto wa kike, Vyoo, Vifaa vya kufundishia na kujifunzia, Upatikanaji wa chakula mashuleni.

Alisema, walimu wenye kukidhi mahitaji ya Shule ni muendelezo kwani katika Halmashauri hiyo ulianza kutekelezwa toka mwaka 2017 ambapo mwaka 2017/18 zaidi walikuwa wanafuatilia katika shule za Sekondari kwa kata 16 na mwaka huu 2019 wameanza kwa shule za Msingi kwenye kata tano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!