KATIKA kurahisisha utambuzi wa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika vituo vya kutolea huduma na kudhibiti vitendo vya udanganyifu, Mfuko umejipanga kuanza kutumia Mfumo wa kuwatambua wanachama wake kwa kutumia sura na alama za vidole. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Hatua hizo zimeelezwa leo Alhamisi tarehe 23 Februari 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga, katika mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Waganga Wakuu wa Wilaya na Waganga Wafawidhi wa Vituo nchini unaofanyika Mkoani Dodoma.
“Ili kwenda na kasi ya ongezeko la idadi ya wanachama katika kuwahudumia kwa haraka, kulipa kwa wakati madai ya watoa huduma na wingi wa vituo, Mfuko unalazimika sasa kuhakiki wanachama wake kwa kutumia sura na alama za vidole,” amesema Konga.
Aidha amesema kuwa uwasilishaji, uchakataji na ulipaji wa madai utafanyika kwa njia ya Kielektroniki (e-Claims and online submission) ambapo itasaidia kupunguza matumizi ya fomu.
Pia amesema madai yatalipwa kwa njia ya kielektroniki moja kwa moja katika akaunti za vituo (e- Claims Payment) ili kuondoa malalamiko ya ucheleweshaji wa madai.
Leave a comment