May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watatu mbaroni tuhuma za mauaji

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Ulrich Matei

Spread the love

 

WATU watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, kwa tuhuma za kumuuwa Elizabeth Mwaike. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 29 Mei 2021 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei, akizungumza na wanahabari mkoani humo.

Watuhumiwa wanaoshikiliwa ni, Lusajo Mwaijobelo (32), Naboti Sanga (44) na Christina Chaula (50), ambao ni wakazi wa Kisyosyo-Matema wilayani Kyela mkoani Mbeya.

Kamanda Matei amesema, watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 28 Mei mwaka huu, katika Kijiji cha Kisyosyo mkoani humo.

Kamanda Matei amesema, watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika katika tukio la mauaji lililotokea tarehe 11 Mei 2021, kwenye machimbo ya kokoto ya kampuni ya kichina inayojenga Kituo cha Forodha cha Kasumulu.

Ambapo mwili marehemu Mwaike, uliokotwa katika maeneo hayo ukiwa na majeraha maene ya kichwani baada ya kupigwa na kitu kizito.

“Mwaike alikutwa eneo hilo akiwa ameuawa kwa kupigwa kitu kizito kichwani, umbali wa mita 500 kutoka nyumbani kwake huku chanzo cha tukio hilo kikielezwa kuwa ni wivu wa kimapenzi,” amesema Kamanda Matei.

Kamanda Matei amesema, watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio hilo kukamilika.

“Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani,” amesema Kamanda Matei.

error: Content is protected !!