July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watatu mbaroni tuhuma kumjeruhi mtendaji Kata Morogoro

Pingu

Spread the love

 

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogogo nchini Tanzania linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumshambulia Geoge Kaloya, ofisa mtendaji wa Kijiji ya Chilombira wilayani Mahenge kwa kitu chenye ncha kali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogogo, Fortunatus Musilim akizungumza na MwanaHALISI Online amesema watuhumiwa hao walimshambuliwa Kaloya tarehe 17 Juni 2022 katika eneo la Katope alipokwenda kutekeleza majukumu yake ya kazi akikaimu nyadhifa ya Mtendaji wa Tarafa ya Ruaha.

Kamanda Musilim amesema ofisa huyo alikuwa akiwaondoa wachimbaji madini wasiokuwa na vibali kwenye eneo la Kitope ndio watuhumiwa hao wakamshambuliwa.

Amewataja wanaoshikiliwa Twaiba Masikini (56) mkazi wa Kijiji cha Togo, Osward Sixbelt (36) na William Ali (65) kwa tuhuma za kumjeruhi Ofisa huyo.

Ofisa huyo amelazwa Hospitali ya St. Fransics ya Ifakara akiendelea na matababu.

“Upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani watuhumiwa hao,” amesema Kamanda Musilim.

error: Content is protected !!