June 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Watanzania wengi ni wavivu – Mavunde

Spread the love

ASILIMIA 71 ya watanzania wanatumia muda wao kufanya mambo yasiyo na tija ambayo hayasaidii katika ujenzi wa taifa na maendeleo yao kiujumla, anaandika Regina Mkonde.

Hayo yamesemwa na Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Ajira, Kazi na Vijana wakati akizindua huduma ya ‘tiketi rafiki’ ambayo ni mfumo wa ukataji tiketi za mabasi kwa kutumia simu za mikononi, jijini Dar es Salaam.

“Asilimia 71 ya watanzania wanatumia muda wao kufanya mambo yasiyo na tija kwenye kuijenga nchi pamoja na maendeleo yao kwa ujumla,” amesema na kuongeza;

“Katika dunia ya leo nguvu kazi ni vijana lakini kwa bahati mbaya wengi wanatumia simu za kisasa kujifurahisha badala ya kufanya kazi. Mitandao ya kijamii inatumiwa kutukanana, kutumiana picha na mambo mengine mengi yasiyo ya msingi.”

Mavunde amesema kuwa, mfumo huo wa ukataji tiketi za mabasi ya mikoani kwa njia ya simu za mikononi utasaidia wananchi kuokoa muda wao.

“kwa takwimu tulizonazo, kati ya watu milioni 44 nchini, milioni 32 wanatumia simu za mkononi na kwahiyo hawa wanaweza kuutumia mfumo huu ili kuokoa muda wao,” amesema Mavunde.

Raymond Magambo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Light nchini, amesema kuwa ‘tiketi rafiki’ itasaidia kupunguza matukio ya utapeli yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya mawakala feki wa mabasi ya mikoani.

“Wananchi wengi wamekuwa wakitapeliwa fedha zao na mawakala wadanganyifu katika vituo vya mabasi, mfumo huu ni halali na unatambulika na wamiliki wa mabasi hivyo si rahisi abiria kutapeliwa na au kupandishiwa bei katika msimu wa siku kuu,” amesema Magambo.

 

error: Content is protected !!