August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watanzania wawagomea Wachina

Spread the love

 

WAFANYAKAZI 170 wa Kampuni ya Ujenzi ya China Railway Jianchang Engineering (CRJE), wameingia katika mgomo usio na kikomo wakishinikiza uongozi wa kampuni hiyo kuwalipa stahiki zao, anaandikaMoses Mseti.

Kampuni ya CRJE iliyopewa tenda ya kujenga hoteli ya nyota tano katika eneo la Kapripoint na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) tangu mwaka 2013, inatuhumiwa na wafanyakazi na vibarua hao kwamba, inawalipa fedha kidogo.

Wafanyakazi hao wameanza mgomo huo leo asubuhi wakigomea kulipwa Sh. 10000 badala ya Sh. 12500 kama ilivyoidhinishwa na serikali.

Pia wanaituhumu kampuni hiyo kwamba, imekuwa ikiwakata fedha kutoka kwenye mishahara yao kwa madai ya kuwapelekea NSSF lakini hazipelekwi.

Baadhi ya wafanyakazi hao wakizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo hilo lililopo Kapripoint wamesema kuwa, wanashangazwa na uongozi wa kampuni hiyo kushindwa kuwalipa kiasi hicho tangu mwaka 2013.

“Kama Rais John Magufuli anatusikia, tunamuomba awatimue hawa wageni wanaokuja kutunyanyasa kwenye nchi yetu, sisi ndio tunajenga ghorofa hili, wao kazi yao ni kutusimamizi tu.

“Mshahara wetu ni kidogo, kwa siku unalipwa Sh. 10,000 na ikipelekwa NSSF inakatwa, tukifuatilia huko wanakozipeleka wanatuambia hele zetu hazijawekwa, tutaishije sisi,” amesema Hussein Amir.

Li Bo, Meneja Mradi wa Kampuni amesema kuwa, wanatarajia kulipa mapunjo ya mishahara ya wafanyakazi pamoja na vibarua wote wanaoidai kampuni ikiwa ni jumla ya Sh. 50 milioni.

“Kuanzi leo tutaanza kutatua migogoro ya wafanyakazi wetu na vibaru wote, kampuni imeanza kufanya mchakato wa kuangalia mapungufu haya ni lazima tufanye kazi kwa kufuata sheria za nchi zinavyoelekeza,” amesema Li.

 

error: Content is protected !!