August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watanzania wapewa somo hati ya kusafiria

Spread the love

IDARA ya Uhamiaji imesema hati ya kusafiria ni haki ya kila Mtanzania ambaye anakidhi vigezo vya kuimiliki na inatolewa na serikali siyo matapeli wa mitaani, anaandikaMwandishi wetu.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Uhamiaji mkoa wa Dodoma, Peter Kundy, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho ya wakulima na wafugaji nanenane kanda ya kati yaliyofanyika  kwenye viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.

Kundy amesema kuwa licha ya kuwa hati ya kusafiria ni haki ya kila Mtanzania, lakini mwananchi huyo ni lazima awe amekidhi vigezo vinavyohitajika kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Hata hivyo, amesema wananchi wanatakiwa kuwa makini na baadhi ya watu ambao ni matapeli wanaojifanya kuwa ni maofisa Uhamiaji wakati ni uongo.

Amesema hati za kusafiria hupatikana katika ofisi za idara ya uhamiaji baada ya mtu  kujaza fomu maalumu ambazo kwa sasa zinapatikana nchi nzima.

error: Content is protected !!