January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watanzania wachagueni viongozi wazalendo

Mkazi wa Kigoma Ujiji

Spread the love

ASKOFU Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Mungu, Lazaro Mayala, amewataka watanzania kuhakikisha wanawachagua viongozi ambao wanauzalendo wa kuwaondoa watanzania katika dimbwi la umasikini. Anandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo askofu huyo amesema umefika wakati wa kuhakikisha kiongozi anayechaguliwa anasimamia vyema rasilimali za taifa na zinawanufaisha watanzania wote.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa kuwachagua viongozi mbalimbali kwa ngazi ya askofu Mkuu,Makamu askofu mkuu na Katibu Mkuu.

Askofu Mayala amesema kwa sasa hali ya kisiasa nchini si shwari kutokana na kuwepo kwa viashiria vingi hususani wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Tumejaribu kufuatilia mambo mbalimbali wakati wa kura za maoni jambo kubwa lililoonekana kutawala ni malalamiko ya wagombea wao kwa wao wakilalamika kuhusu na kuhujumiana” amesema .

Mbali na hilo askofu huyo alisema watanzania wanatakiwa kuachana na ushabiki wa kuwachagua viongozi kutokana na ushawishi wa rushwa .

“Tumefika hapa tulipo kutokana na wananchi wengi kutokuwa makini katika uchaguzi wa viongozi, tusipokuwa makini katika kuwachagua ambao wanakemea rushwa na ubadhilifu wa mali za Umma”amesema

Akizungumza kuhusu huduma za kijamii amesema kanisa hilo limekuwa litikoa elimu ya ujasiliamali kwa akina mama na vijana kwa lengo la kujikomboa kiuchumi.

Katika uchaguzi huo waliochaguliwa ni Askofu Mkuu Sebastian Micheli, Makamu wake ni Timotheo Mtobora na Katibu mkuu ni Richison Kalinga.

error: Content is protected !!