January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watanzania tumieni changamoto kuwa fursa

Mkuu wa wilaya ya Arusha, Christopher Kangoye (kushoto) akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Ngarenaro jiji la Arusha, Isaya Doita

Spread the love

WATANZANIA  wametakiwa kuwa wabunifu  na kuzibadili changamoto kuwa fursa inayoweza kuwakomboa kuwatoa katika lindi la umasikini na kukuza uchumi wao. Anaandika  Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea).

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Christopher Kangoye amesema kuwa mchango wa wabunifu na wanasanyansi unaweza kubadili changamoto na kuwa fursa zitakazowanufaisha watu kiuchumi badala ya kubaki kuzilalamikia.

Akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya wiki ya Mandela inayofanyika  katika Chuo Kikuu cha  Sayansi Teknolojia cha Nelson Mandela  amesema kuwa bila kuwa na wanasayansi wa kutosha tutaendelea kuziangalia changamoto kama matatizo wakati ni fursa zinazoweza kubadilisha maisha ya watu wengi.

Makamu Mkuu wa taasisi hiyo Profesa Burton Mwamila amesema, katika maadhimisho hayo  yanalenga kuchochea ubunifu na ugunduzi unaofanywa na wanasayansi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Amesema  ni njia moja wapo ya kumuenzi Hayati Nelson Mandela ambae ndio muasisi wa taasisi hiyo ya elimu ya juu na mwanamapinduzi aliehimiza sayansi katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi barani Afrika.

Kwa  upande wao baadhi ya washiriki wa kongamano hilo akiwemo Mhadhiri wa chuo hicho Dk.Askwar Hillonga  na Carren Faustine mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Usariver Academy  amesema ni wakati sasa ya wasomi na wanasayansi kuhakisha kuwa wanazitumia taaluma zao katika kubadilisha maisha ya watanzania walio wengi.

Wanafunzi wengi wamejijengea mtazamo kuwa masomo ya sayansi ni magumu jambo ambalo linawaathiri   masomo ya sayansi na ninayafurahia, anaeleza Carren

Amesema  iwapo masomo ya Sanyansi yatatiliwa mkazo na taasisi za elimu nchini ni wazi kuwa pengo la uhaba wa wataalamu wa Sayansi litazibwa hivyo kuchochea maendeleo katika kila sekta.

error: Content is protected !!