July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watanzania kujifunza tamaduni za kichina

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa amewataka Watanzania kujifunza lugha ya kichina na utamaduni wake ili kukabiliana na fursa za kiuchumi za taifa hilo lililoendelea kiuchumi duniani. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Amesema hayo katika tamasha la kubadilishana tamaduni za kichina lililofanyika Ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma.

Maonyesho hayo yaliyoratibiwa na taasisi Confucius ya UDOM (CIUDOM) ambayo yalijumuisha maonesho ya picha na vifaa mbalimbali vya asili ya utamaduni wa China, namna ya kusoma na kuandika tarakimu za kichina, uimbaji nyimbo za kichina na uchezaji michezo mbalimbali kama Konf fuu pamoja na ukuzaji jinsi ya kuongea lugha ya kichina ili kuongeza uelewa wa watu wa mataifa mengine kuijua lugha hiyo na kuongeza uelewa zaidi wa mambo ya kimataifa.

Mkurugenzi Mkazi wa taasisi hiyo tawi la UDOM, Dk Ajali Mustafa amesema kuna umuhimu kwa Watanzania kujifunza lugha na tamaduni za China.

Amesema hilo litasaidia kuongeza uelewa wa kutambua fursa zitakazotoa majibu ya matatizo ya ajira kwa vijana hasa wanapomaliza masomo yao na kutumia vyema fursa nyingi za kibiashara nchini China duniani kote.

Amesema taifa hilo kwa kipindi hiki limedhamiria kuongeza na kukuza mahusiano yake na mataifa mengine duniani.

Pia aliwashauri watu wa rika mbalimbali kuanza kujiunga na madarasa ya ufundishaji lugha hiyo.

Washiriki mbalimbali waliohudhuria maaonyesho hayo walivutiwa sana na mpango huo hasa baada ya kuangalia maonyesho ya uimbaji na uchezaji wa nyimbo za kichina, wanafunzi wengi wa shule za sekondari na msingi hapa Dodoma walivutiwa na ufasaha wa uimbaji wa kichina ujulikanao kama “Chinese Karaoke.”

error: Content is protected !!