
WATANZANIA watatu kutoka visiwani Zanzibar, Idarous Abdirahman (32), Islah Juma (22) na Mbarouk Adibu (34) wamefungwa miaka 15 jela kila mmoja nchini Kenya, kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya ugaidi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Watuhumiwa hao walikamatwa na maafisa usalama wa Kenya mwaka 2018 maeneo ya Kutulo nchini humo wakivuka mpaka kwa ajili ya kuingia nchini Somalia, wakiwa na silaha zilizotumika kwenye vitendo vya kigaidi.
Walihukumiwa kifungo hicho jana Jumatano tarehe 30 Januari 2019 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu Wajir mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amos Makoros.
Kabla ya hukumu hiyo, watuhumiwa hao waliwekwa katika gereza la Wajir tangu tarehe 19 Oktoba 2018 wakati polisi walipokuwa wakifanya uchunguzi wa kesi yao. Kwa sasa watatumikia kifungo chao katika gereza hilo.
More Stories
Kifo cha mtawa: Ni simulizi nzito
TAKUKURU: Rushwa ya ngono ipo, fichueni
Usiyoyajua kuhusu Panya wapima TB