Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Watanzania 6 kuchuana taji la Miss Dunia 2022
Habari

Watanzania 6 kuchuana taji la Miss Dunia 2022

Spread the love

 

Tanzania imepata nafasi ya kupeleka washiriki sita kwenye Fainali za Urembo, Mitindo na Utanashati kwa viziwi ya ngazi ya dunia yatakayofanyika Aprili 2022 nchini Brazil. Anaripoti Mwandishi wetu (endelea…)

Hatua hiyo imekuja kutokana na ushindi wa washiriki wake wawili waliofanya vizuri kwenye fainali za Afrika zilizomalizika Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Oktoba mwaka huu.

Taarifa kuhusu ushiriki huo, imetolewa leo tarehe 3 Oktoba na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, John Mapepele.

Imesema katika shindano hilo  la kwanza kufanyika Afrika na Tanzania kuwa mwenyeji, washiriki wa Tanzania walioshinda ni Khadija Kanyama aliyeshika nafasi ya pili Afrika (Kundi la Miss Deaf Afrika 2021) na Carloyne Mwakasaka (Kundi la Miss Deaf Africa – Fashion) aliyekuwa mshindi wa kwanza.

“Kutokana na ushindi huo Kamati ya Kimataifa ya Mashindano hayo imetoa taarifa ya washiriki wengine wanne kutoka Tanzania ambao sasa nao wamekidhi vigezo vya kushiriki mashindano hayo kwa ngazi ya dunia kuwa nl Surath Mwanis, Rajani Ali na Russo Songoro upande wa Mavazi na Mitindo huku Joyce Denis akipata nafasi ya kushiriki katika eneo la urembo.

“Jumla ya washiriki 8 wa Tanzania waliungana na washlriki wengine zaidi ya 30 kutoka nchl nyingine 12 za Afrika,” imesema.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Mashindano hayo kidunia ambaye pia alikuwa Jaji Mkuu wa shindano hilo la Dar es Salam, Artur Dzerbis, ameipongeza Serikali kwa kuandaa mashindano haya katika kiwango cha juu kwa kuwa ndio yamefanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika.

Pia ameeleza kuwa Kamati ya Dunia imeridhishwa na kiwango hicho.

Wakati huo huo, Makamu huyo wa Rais amesema Kamati yake imepokea maombi ya Serikali ya Tanzania yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Hassan Abbas kuhusu utayari wa Tanzania kuendelea kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa ngazi ya Bara la Afrika kwa miaka nitatu zaidi.

Amesema ombi hilo litawasilishwa wa kwenye Kamati ya Kimataifa na kutolewa uamuzi kwani Tanzania imeonesha uzoefu na uwezo mkubwa kupitia shindano hilo la kwanza.

Kwa upande wake, Dk. Abbas amewaomba wadau mbalimbali kuwasaidia washiriki hao wa Tanzania ili kuwawezesha kujiandaa vyema na kufanya vizuri zaidi huko Brazil iii kuileteasifa nchi yetu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!