May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watanzania 33,000 waugua Corona, 781 wafariki

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imesema hadi kufikia tarehe 23 Januari, 2022 jumla ya Watanzania 33,000 wamethibitika kuwa na maambukizi na watu 781 wamepoteza maisha. Anaripoti Danson Kaijage,  Dodoma … (endelea).

Aidha, imeeleza kuwa tangu ianze kutoa chanjo dhidi ya UVIKO-19 nchini hadi sasa jumla ni dozi 8,821,210 aina za Sinopharm, Janssen, Moderna na Pfizer ambazo zinatosha kuchanja jumla ya watanzania 5,082,380.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwa na Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian wakati wa kupokea chanjo za UVIKO-19 aina ya Sinopharm dozi 800,000 kutoka nchini China.

Akipokea chanjo hizo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassani, Waziri huyo ameishukuru Serikali ya China kwa kuipatia Tanzania chanjo hizo.

Amesema chanjo hizo ni awamu ya pili, awamu ya kwanza walipokea jumla ya dozi 500,00 ambazo zilitumika kuchanja wananchi 250,000.

“Takwimu za tarehe 25 Januari, 2022 jumla ya watu 1,922,019 sawa na asilimia 3.33 ya watanzania walikuwa wamepata chanjo kamili” ameeleza Ummy.

error: Content is protected !!