January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watanzania 23 wahifadhiwa A. Kusini

Raia wa Afrika kusini wakimshambulia, raia wa kingeni

Spread the love

TANZANIA imesema haina takwimu za idadi rasmi ya Watanzania waishio nchini Afrika Kusini – nchi ambayo imekubwa na machafuko ya uvamizi kwa wegeni wanaotoka mataifa ya Afrika. Anaandika Pendo Omary(endelea)

Wakati idadi idadi hiyo ikiwa tata, tayari watu 8 kutoka mataifa ya Ethiopia, Malawi, Zambia, Malawi na Swazland wamekufa kutokana na machafuko hayo.

Mbali na vifo hivyo, raia wa kigeni 3,000 wamehifadhiwa katika kambi ya Isipingo iliyopo katika mji wa Durban.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam, Bernard Membe – Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, amesema, “idadi ya Watanzania wanaoishi Afrika Kusini haijulikani”.

“Hatuna takwimu sahihi kuhusu ni wangapi wanaishi huko. Wengi wanaenda kwa njia za panya. Katika miji ya Durban na Johannesburg pekee wapo watanzania wanaokadiliwa kufikia 10,000,”amesema Membe.

Aidha, Membe amesema wapo watanzania 23 kati ya watu 3000 waliohifadhiwa katika kambi ya Isipingo. Tayari Tanzania imefanya mazungumzo nao ambapo 21 wamekubali kurudi nyumbani huku wawili kakikataa kurejea.

Pia Membe amekanusha taarifa zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii kwamba “kuna watanzania watatu wamekufa kufuatia machafuko hayo”.

“Ni kweli kuna watanzania watatu wamekufa nchini humo. Na majina yao ni haya; Rashidi Jumanne – huyu aliuwawa Kilomita 90 kutoka Durban. Aliuwawa akiwa kwenye kitendo cha unyang’anyi,” amesema Membe

Ameongeza kuwa mtanzania mwingine ni Athuman China – Huyu alifugwa baada ya kufanya makosa ya jinai. Aliuwawa kwa kupigwa visu katika gereza la Westville lilipo Durban baada ya kuibuka mapigano baina ya wafugwa.

Pia mtanzania Ally Heshima Mohamed – amefia katika hospitali ya Johannesburg baada ya kuugua ugojwa wa TB miezi miwili iliyopita na mwili wake umerejeshwa nchini jana.

“Nimezungumza na Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini, nimemuita Balozi wa Tanzania chini kwa mazungumzo na nimezungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini. Swali kubwa nililowauliza ni “tumepoteza watanzania wangapi katika mgogoro huo?” nimehakikishiwa hatujapoteza hata mtu mmoja,” amefafanua Membe.

Kuhusu hatua iliyochukuliwa na serikali ya Afrika Kusini katika kukomesha machafuko hayo, Membe ameongeza kuwa, tayari amepewa taarifa kwamba saa 48 zilizopita hali ya usalama nchini humo imeanza kuimalika huku watuhumiwa watatu wa mauji ya raia wa Msumbiji wakikamatwa.

Membe ameongeza kuwa Kamati ya kushughulikia tatizo hilo imeudwa huku Rais Jacob Zuma akihairisha safari yake nje ya nchi yake ambapo amewatembelea raia wa kigeni waliohifadhiwa katika kambi ya Isipingo.

Mbali na kutembelea waathirika wa machafuko hayo, Zuma amekutana na  Mfalme wa kabila la Zulu, Goodwill Zwelithini, ambaye anadaiwa kutoa matamko yaliyochochea vurugu hizo. Na sasa Zwelithini anafanya jitihada kwa kuzungumza na raia kuacha mashambilizi dhidi ya wageni.

Kuhusu msimamo wa Tanzania juu ya machafuko hayo, Membe amesema, “Tanzania inaungana na Robert Mugabe – Rais wa Zimbabwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADEC) na Umoja wa Afrika (AU) ambaye ametoa tamko la kulaani machafuko hayo.”

error: Content is protected !!