Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Watano mbaroni kwa tuhuma za mauaji Dar
Habari Mchanganyiko

Watano mbaroni kwa tuhuma za mauaji Dar

Kamanda Wambura
Spread the love

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu watano, wanaotuhumiwa kumuuwa aliyekuwa mlinzi wa Baa, Regan Sylvester. Anaripoti Jemima Samweli, DMC…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne tarehe 25 Mei 2021, na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP, Camilius Wambura, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Kamanda Wambura amewataja watuhumiwa hao kuwa ni, Issa Kari maarufu kama Mdaka Bomu (33), mkazi wa Mbezi . Mohamed Juma ‘Mabangi’ (31), mkazi wa Mbezi Mwisho na Selemani Seif ‘Dullah Kishandu’ (34), mkazi wa Mbezi Mwisho.

Wengine ni, Samsoni Joseph ‘Mjeuri’ ( 32), mkazi wa Mbezi na Ezekiel Kennedy ‘Simba MC’, mkazi wa Mbezi.

Watuhumiwa hao wanaidwa kufanya mauaji hayo usiku wa tarehe 8 Mei 2021, maeneo ya Mikocheni A, baada ya kuvamia Baa inayofahamika kwa jina la Imbizo, kisha kumshambulia mlinzi huyo kwa mapanga hadi kufa.

“Mnamo tarehe 08 Mei 2021 majira ya 8:05 usiku huko Mikocheni A, watuhumiwa hawa walivamia katika baa iitwayo Imbizo na kumshambulia kwa mapanga na marungu mlinzi aliyefahamika kwa jina Regan Sylivester na kusababisha kufariki dunia papo hapo,”amesema Kamanda Wambura.

Wakati huo huo, Kamanda Wambura amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha, lililotokea tarehe 7 Mei mwaka huu, maeneo ya Mabwepande, mkoani Dar es Salaam.

“Tarehe 07 Mei 2021 majira ya 09:00 usiku, walivamia katika kituo cha kuuzia Mafuta (Petrol station) cha MEXONS na kuwashambulia walinzi, wahudumu na wateja na kupora kiasi cha Sh. 2, 440,000. Kisha kupora silaha aina ya Short Gun ya walinzi hao,” amesema Kamanda Wambura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

error: Content is protected !!