Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Watakiwa kutotumia nafaka kutengeneza pombe
Habari Mchanganyiko

Watakiwa kutotumia nafaka kutengeneza pombe

Mwananchi akianika ulezi kwa ajili ya kutengenezea pombe
Spread the love

MUSTAFA Rajabu Sheikh wa Mkoa wa Dodoma na Kadhi wa Mkoa huo amewaasa Watanzania kutotumia nafaka kama mahindi na mtama kwaajili ya kutengeneza pombe za kienyeji ilihali kuna uhaba wa chakula uliosababishwa kuchelewa kwa mvua, anaandika Dany Tibason.

Sheikh Mustafa ameyasema hayo alipokuwa ikitoa mawaidha katika ibada ya  leo Ijumaa katika msikiti wa Gadafi mjini hapa.

Mbali na hilo pia, sheikh huyo amewataka wananchi kutumia vyema mvua zinazonyesha kwa kupanda mazao ya muda mfupi na yasiyohitaji mvua kubwa.

“Viongozi wa dini mbalimbali tulifunga na kuomba ili mvua iweze kunyesha, na maombi hayo yamejibiwa kwani mvua zimeanza kunyesha hivyo ni wajibu wa Watanzania kutumia mvua hizo kwaajili ya kupanda mazao ya muda mfupi.

“Wakulima waachane na tabia ya kuuza mazao yakiwa shambani na badala yake wavute subira ili waweze kuvuna na wauze kwa vipimo ambavyo vinastahili,” amesema.

Katika hatua nyingine Sheikh Mustafa amewataka watawala hapa nchini kuhakikisha wanasimamia haki katika utendaji wao wa kila siku.

“Vitabu vyote vitakatifu vinahimiza utoaji wa haki hivyo ni lazima viongozi wote wenye mamlaka wasimamie haki bila kuwaonea wenzao au kuwatengenezea majungu kwa nia ya kuwakomoa.

“Vyombo vyote vinavyohusika katika utoaji haki lazima vitende haki, mabaraza yote ya maamuzi lazima yasimamie haki kwani haki ndiyo inaweza kuliweka Taifa katika hali ya usalama zaidi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!