January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Watakiwa kuandika makala za kilimo’

Spread the love

WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imetoa rai kwa waandishi wa habari wanaoandika makala za uzalishaji wa bidhaa za mifugo kuwasiliana na wataalamu bigwa wa mifugo waliopo wizarani ili kupata elimu zaidi, anaandika Happyness Lidwino.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Aron Luziga, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Uzalishaji amesema, wizara imetoa rai hiyo kwa kuwa waandishi wanadhamana kubwa katika kuelimisha jamii.

Pia amesema waandishi wakishirikiana na wizara hiyo na kuandika habari za uhakika, watasaidia kulinda soko la bidhaa zinazozalishwa nchini kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi na kuwaondolea umaskini wafugaji, wafanyabiashara pia kukuza pato la taifa.

Luziga pia amezungumzia faida za mifugo nchini ambapo amesema, inachangia upatikanaji wa ajira, lishe, nishati, mbolea pamoja na kuwaingizia fedha za kigeni wafugaji na taifa kwa ujumla.

Amesema, kulingana na takwimu zilizopo idadi ya mifugo nchini inakadiriwa kuwa ni ng’ombe milioni 25.8, mbuzi milioni 16.7 na kondoo milioni 8.7. Kuku wa kisasa milioni 32.0 na wa asili milioni 37.0 huku nguruwe wakiwa milioni 2.5.

Aidha, mwaka 2014 na mwaka 2015 wafugaji waliuza minadani jumla ya ng’ombe 1,337,095, mbuzi 1.056,218 na kondoo 230,221wenye thamani ya Sh. 1,027.4 bilioni.

Mbali na hilo Luziga pia amezungumzia suala la unenepeshaji wa mifugo ambapo kabla ya kuuzwa kwa ajili ya kuchinjwa, huandaliwa kwenye eneo moja na kulishwa vyakula vyenye wanga na protini kwa wingi kwa siku 90 hadi 120 ili kuzalisha nyama yenye ubora.

Lengo la unenepeshaji huo amesema ni kupata nyama uzito, nyama kuwa laini na yenye radha nzuri.Mifugo hiyo huandaliwa kwa kupatiqa kinga za magojwa mbalimbali ikiwemo minyoo.

Hivyo, Mkurugenzi huyo amewataka wananchi kutoa hofu wakati wa matumizi ya nyama iliyonenepeshwa kwa kuhofia kupata magojwa kwani zoezi hilo ni moja kati ya mikakati ya kuendeleza sera ya taifa ya mifugo ya mwaka 2006.

error: Content is protected !!