Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Watakaofanya ukatili wa kijinsia kutokupata dhamana
Habari Mchanganyiko

Watakaofanya ukatili wa kijinsia kutokupata dhamana

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwanaid Khamis
Spread the love

 

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu  imejipanga kuweka mkakati kwa wale wote wanaofanya ukatili wa watoto na wanawake wasipate dhamana ili kuzuia kufanya matukio mengine wakiwa uraiani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Hayo yamesemwa na jana tarehe 2 Agosti, 2022 Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mwanaid Khamis kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi wakati akipokea taarifa ya Wilaya hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya, Jerry Muro.

Mwanaid amesema kuwa mkakati huo utajikita na kuweka sheria ya kutokuwapatia dhamana kwa mtu yeyote atakayefanya ukatili wowote kwa wanawake na watoto nchini ili wale wanaofanya matukio hayo wasipate dhamana ili kuepusha matukio mengine pale watakapokua uraiani.

“Inasikitisha sana na ukatili unaoendelea hivi sasa nchini, nina imani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote wanaofanya  matukio ya kikatili ikiwemo ya kutoa uhai.”

Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri huyo, Jerry Muro alisema Wilaya yake imejikita kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa kushirkiana na Mabalozi wa SMAUJATA hususan kipindi hiki cha mavuno ambapo kumekuwepo na matukio ya mauaji ya wanawake katika maeneo ya vijijini.

Alisema ukatili wa watoto na wanawake bado unaendelea na kama Wilaya bado  wanaendelea kutoa mkazo kwa kuwatafuta waharifu na kuwakamata ili sheria zichukue mkondo wake.

“Tunapambana nao wale wote wanaofanya ukatili kwa watoto na wanawake tunahakikisha tunawakamata, tangu matukio haya  yanayotokea kwenye Wilaya yetu tumewakamata wale wote wanaofanya ukatili huu na tunazidi kutoa elimu na Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii.”

Hivi karibuni wanawake wawili kutoka vijiji tofauti katika Wilaya ya Ikungi wameuliwa kikatili na wanaume zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!