August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watakao kwamisha mradi wa kuboresha Elimu Sekondari kukiona

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Spread the love

 

NAIBU Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Davidi Silinde,amesema kwa uzembe wowote utakaofanyika kwa na kukwamisha mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) muhusika atachukuliwa hatua kali za kisheria. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kutokana na onyo hilo Silinde ametoa angalizo kwa watendaji hao kwa kueleza kuwa yoyote ambaye atajaribu kukwamisha mradi huo hataweza kuvumiliwa na kabla hajachukuliwa hatua ni lazima ajitafakari.

Baada ya kusema hayo Silinde ameeleza kuwa Serikali kupitia mradi wa kuboresha Elimu Sekondari (ESQUIP) katika mwaka wa fedha 2020/22 imetumia fedha kwenda Mamlaka za Serikali za Mitaa takribani Sh139.57 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za sekondari 243 zikiwemo 10 za bweni za Mikoa kwa ajili ya wasichana na shule 232 za kata katika kata ambazo hazina shule na kata zenye wanafunzi wengi ukilinganisha na miundombinu ya shule iliyopo.

Hayo yamebainishwa jana Juni 29 mwaka huu na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), David Silinde wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo maofisa mazingira kuhusu masuala ya usalama wa Mazingira na Jamii katika kutekeleza mradi wa SEQUIP yaliyofanyika jijini Dodoma.

Silinde amesema kuwa utekelezaji wa Mradi huo ni kwa ajili ya kutatua changamoto ya ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa katika shule za sekondari nchini kutokana na utekelezaji wa sera ya elimu bila maipo.

“Sera hiyo imesababisha kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari.

“Mfano katika mwaka 2021 wanafunzi wa elimu ya awali,msingi na kidato cha kwanza walikuwa 3,469,275 ambapo kumekuwa na ongezeko la wanafunzi 472,969 walioandikishwa mwaka 2022 na kufikia wanafunzi 3,942,244 sawa na ongezeko la asilimia 14.

“Mradi huu wa SEQUIP umekuja wakati ambapo kumekuwa na mwitikio mkubwa katika uandikishaji wa wanafunzi na hivyo kusababisha ongezeko la Mahitaji ya miundombinu kwa ajili ya kupokea wanafunzi wanaijiunga na Elimu ya Sekondari” ameeleza Silinde.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu Tamisemi, Ephraim Simbeye kwa niaba ya Naibu Karibu Mkuu Tamisemi Dk.Charless Msonde, wakati akitoa maelezo mafupi katika mafunzo hayo amesema kuwa miradi wa SEQUIP unatarajiwa kutekelezwa katika eneo la Elimu ya Sekondari kidato cha kwanza hadi cha sita kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2020/2021hadi 2024/2025.

Amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa utaratibu wa lipa kulingana na matokeo ambapo motisha ya fedha hutolewa kwa Serikali baada ya kufikia matokeo yaliyokubalika kwa kuzingatia viashiria vya mradi.

Aidha Simbeye amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo unatarajia kuleta mafanikio na maboresho makubwa katika eneo la Elimu ya sekondari ikiwemo kuwasaidia wanafunzi milioni 6.5 kumaliza elimu ya sekondari na stadi za maisha,kati yao wanafunzi wasichana milioni 3.2 wakiwemo wasichana waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali.

error: Content is protected !!